• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
Kalonzo, Mudavadi wamtetea Uhuru

Kalonzo, Mudavadi wamtetea Uhuru

LEONARD ONYANGO na VALENTINE OBARA

VIONGOZI wa kisiasa Jumapili walimtetea vikali Rais Uhuru Kenyatta kwa juhudi zake za kupambana na ufisadi, huku wakikemea wanaohujumu juhudi hizo.

Kiongozi wa Chama cha Wiper, Bw Kalonzo Musyoka na mwenzake wa Amani National Congress (ANC), Bw Mudalia Mudavadi walitoa wito kwa wananchi kupuuza wanaopinga vita dhidi ya ufisadi.

“Tunahimiza Mkurugenzi wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu na Mkuu wa Mashtaka ya Umma kuhakikisha kuwa wezi wote wanachukuliwa hatua kali za kisheria,” akasema Bw Musyoka.

Alikuwa akizungumza wakati chama hicho kilipomtangaza aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Bw Chirau Ali Mwakwere kuwa mwenyekiti mpya kuchukua mahali pa Gavana wa Makueni, Prof Kivutha Kibwana.

Katika Kaunti ya Nakuru, Bw Mudavadi alisema vita vya ufisadi havifai kuingizwa siasa za kikabila.

“Uhuru lazima aendelee kupambana na ufisadi na Wakenya tumsaidie. Tunaambia wanaoleta ukabila kwamba kabila halikuhusika kwa ufisadi, ni watu binafsi,” akasema.

Kwingineko Kajiado, Naibu Rais William Ruto alizidi kudai wanasiasa wameingilia vita dhidi ya ufisadi akataka asasi husika zipewe uhuru wa kutekeleza majukumu yao.

You can share this post!

Oburu Odinga aikejeli EACC kwa kumpokonya ardhi

Kesi ya kupinga ‘Punguza Mizigo’ kuharakishwa

adminleo