HabariSiasa

Hatutakubali mwili wa Ken Okoth kuchomwa – Wazee

July 31st, 2019 Kusoma ni dakika: 2

 GEORGE ODIWUOR Na BENSON MATHEKA

KUNDI moja la baraza la wazee wa jamii ya Waluo limesema kwamba halitakubali mwili wa aliyekuwa mbunge wa Kibra, Ken Okoth uchomwe wakisema ni kinyume na desturi za jamii yao.

Bw Okoth aliaga dunia wiki iliyopita baada ya kuugua kansa na mama yake amepinga kuchomwa kwa mwili wake.

Mke wa Bw Okoth, Monica na ndugu mdogo wa mbunge huyo, wanataka mwili wake uchomwe. Kulingana na wawili hao, yalikuwa mapenzi ya mbunge huyo mwili wake uchomwe.

Lakini wazee wa jamii ya Waluo wanasema kwamba, kulingana na desturi za jamii yao, kuchoma mwili ni kinyume na desturi za jamii yao.

Kulingana na mzee Nyandiko Ongadi anayeongoza kundi la wazee wa Waluo, Okoth ni mwana wa jamii hiyo na mazishi yake yanapaswa kufanywa kwa kuzingatia utamaduni wao.

“Nilifahamishwa kuwa marehemu mbunge atachomwa kuwa jivu. Hii ni kinyume cha desturi za jamii ya Waluo na Mluo yeyote hafai hata kufikiria jambo kama hilo,” alisema.

Mzee huyo alidai kwamba matamshi ambayo mbunge huyo anadaiwa kutamka yanaweza kuwa yalitokana na mapenzi, lakini mke wa Okoth hawezi kuamua jinsi anavyopaswa kuzikwa.

“Utamaduni wetu unasema kwamba, ikiwa mwana wetu anaoa mwanamke asiye wa jamii, mkewe anapaswa kukumbatia desturi za Waluo,” alisema Bw Ongadi.

Aliwaambia wanasiasa wanaoandaa mazishi washirikiane na baraza hilo ili kuepuka mizozo.

“Haifurahishi kuona mizozo kama hii katika mazishi. Waandalizi wa mazishi wanapaswa kushirikiana nasi kuweka mipango inayofaa,” alisema.

Kulingana na mzee Ongadi, marehemu anapaswa kuzikwa kando ya kaburi la baba yake katika wadi ya Kochia, eneobunge la Rangwe.

Naye mama yake Anjeline Ajwang anataka mwili wa mwanawe kuzikwa katika boma lake Kasewe eneobunge la Kabondo Kasipul.

Bw Ongadi alisema alimtuma mwenyekiti wa tawi la Homa Bay la baraza hilo, Bw Owili Mwai kwa familia ya baba ya mbunge huyo kuuliza atakakozikwa.

Msemaji wa familia hiyo Raymond Mbai alidai kwamba baba ya Okoth, Nicholas Anayo Obonyo alikuwa