Habari Mseto

Shule za upili zawasilisha nyimbo za kuvutia zikihimiza maendeleo

August 9th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na ANTHONY NJAGI

SHULE za upili jana zilifika jukwani kwa kishindo katika Tamasha ya Kitaifa ya Muziki katika Chuo Kikuu cha Kabarak kwa kuwasilisha nyimbo mbalimbali zenye maudhui ya kuvutia.

Katika kitengo cha utunzi wa nyimbo, shule hizo zilihitajika kutunga nyimbo zenye kauli mbiu, “Naona Mapya na Bado” inayohusu masuala yanayofungamana na Ruwaza ya Maendeleo ya 2030.

Shule hizo ziliangazia maudhui mbalimbali kauli mbiu hiyo ambayo ni pamoja na; vita dhidi ya ufisadi na kuwawezesha wananchi kufikia afya kwa wote.

Washindi walikuwa ni wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wasichana ya Bishop Sulumeti wakifuatwa na Shule ya Upili ya Wasichana ya St Monica. Shule ya Upili ya Kisoni ilikuwa nambari tatu, Shule ya Upili ya Wasichana ya Karima (nambari tatu) huku ile ya Wasichana ya Gathirumu ikishikilia nambari tano.

Shule ya Upili ya Wasichana ya Gathirimu ilifurahisha hadhira kwa wimbo wao wenye kichwa “Kenya Yetu”.

Wimbo huo unawahimza Wakenya kuwa makini katika kazi yoyote wanayofanya.