• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:45 AM
Wanafunzi waliotia fora tamashani kumtumbuiza Ruto

Wanafunzi waliotia fora tamashani kumtumbuiza Ruto

Na ANTHONY NJAGI

WANAFUNZI waliotia fora katika Tamasha la Muziki la Kitaifa Jumanne wanatarajiwa kutumbuiza wakuu serikalini wakiongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Naibu wa Rais Dkt Ruto ataandamana na waziri wa Elimu Profesa George Magoha na Katibu wa Elimu Dkt Bellion Kipsang.

Jumatatu wanafunzi waliwasilisha nyimbo na ngonjera zenye maudhui kuhusu maadili. Wanafunzi walihimizwa kuangazia umuhimu wa kufundisha watoto maadili mema wakiwa wangali wachanga.

Walisema kuna haja kwa watoto kuheshimu wakubwa wao. Kitengo kilichojumuisha nyimbo za ushairi kilifadhiliwa na Tume ya Kuajiri Wafanyakazi wa Umma (PSC).

Shule ya Wasichana ya Tengecha iliibuka mshindi katika kitengo hicho. Katika wasilisho lao, wanafunzi wa Shule ya Tengecha walikumbusha watu kuhusu maadili ya zamani ambapo wanafunzi walisimama mwalimu alipoingia darasani.

Siku hizi, wanafunzi wa Tengeha walisema, maadili hayo yameyeyuka. Wanafunzi wanaposalimiwa na mwalimu wao wanajibu: “Poa.”

Shule nyingine zilizoshiriki katika kitengo hicho ni wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Lugulu na St Cecilia Misikhu na Precious Blood Riruta.

Mashairi hayo yalihimiza watumishi wa umma kuzingatia maadili wanapohudumu. Kiburi, wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya St Cecelia walisema, hakifai katika afisi za umma.

Shule ya Upili ya Wasichana ya Bahati waliibuka washindi katika kitengo cha Lugha ya Kiingereza, Kifaransa na Kijerumani.

You can share this post!

Mayatima, maskini wachinjiwa ng’ombe 1,000 sikukuu ya...

Viongozi Rift waikemea serikali kujaribu kufurusha familia...

adminleo