• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 3:23 PM
SJAK yatangaza orodha ya wawaniaji wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka

SJAK yatangaza orodha ya wawaniaji wa tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka

Na GEOFFREY ANENE

ORODHA ya wawaniaji wa Tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka nchini Kenya ya msimu 2018-2019, imetangazwa.

Tuzo hii, ambayo itafanyika Agosti 19, imepata mdhamini mpya kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya LG kwa ushirikiano wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (SJAK) baada ya kampuni ya SportPesa iliondoa ufadhili wake wote nchini Kenya majuzi kutokana na mvutano na serikali.

LG imetangaza Jumanne kudhamini makala ya mwaka huu kwa Sh4 milioni pamoja na kuahidi kuwapa washindi wa vitengo vyote runinga na friji na maikrowevu kwa nambari mbili na tatu.

Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) wa msimu 2018-2019 Enosh Ochieng’ kutoka klabu ya Ulinzi Stars ni mmoja wa wachezaji waliotiwa katika kitengo cha kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka (MVP).

Atapata ushindani mkali kutoka kwa kiungo Francis Kahata, ambaye amehama Gor Mahia katika kipindi hiki kirefu cha uhamisho na kujiunga na miamba wa Tanzania, Simba SC.

Vilevile, kuna beki Joash Onyango (Gor Mahia), mshambuliaji kutoka Uganda Umaru Kasumba, ambaye alielekea nchini Zambia majuzi kutoka Sofapaka, mvamizi matata wa Kakamega Homeboyz Allan Wanga naye nyota wa Tusker FC Boniface Muchiri.

Mbali na kitengo cha mwanasoka bora wa mwaka, kuna vitengo vingine vitano. Kwa sasa, vitengo hivi vina wachezaji sita ambao watapunguzwa hadi watatu hapo Agosti 16.

Orodha kamili ya wawaniaji wa wa msimu 2018-2019:

Kipa Bora

Farouk Shikalo (Bandari/Yanga), Justin Ndikumna (Sofapaka/Bandari), Kevin Omondi (SoNy Sugar), Samuel Odhiambo (Western Stima), Morgan Alube (Chemelil Sugar), Omar Adisa (KCB)

Beki Bora

Joash Onyango, Harun Shakava (Gor Mahia lakini kwa sasa amehamia Enkana ya Zambia), Fainus Jacobs (Sofapaka), Brian Otieno (Bandari), David Owino (Mathare United), Kevin Wesonga (SoNy Sugar)

Kiungo Bora

Abdallah Hassan (Bandari), Cliff Nyakeya (Mathare United), Danson Chetambe (Zoo), Francis Kahata (Gor Mahia), Whyvone Isuza (AFC Leopards), Boniface Muchiri (Tusker)

Chipukizi Bora mpya

David Majak (Tusker), Jackson Dwang (Nzoia), Moses Mudavadi (Bandari), Daniel Sakari (Kakamega Homeboyz), Nixon Omondi (Sharks), Joshua Otieno (SoNy Sugar)

Kocha Bora

Hassan Oktay (aliyekuwa kocha wa Gor Mahia), Bernard Mwalala (Nzoia Sugar), John Baraza (Sofapaka), Robert Matano (Tusker), Patrick Odhiambo (SoNy Sugar), Francis Kimanzi (aliyejiuzulu Mathare United)

Mwanasoka Bora

Francis Kahata (Gor Mahia), Joash Onyango (Gor Mahia), Umaru Kasumba (Sofapaka), Enosh Ochieng (Ulinzi Stars), Allan Wanga (Kakamega Homeboyz), Boniface Muchiri (Tusker)

You can share this post!

Mwanamume afariki kwa kuzidiwa na mahanjamu

Kaunti zajitahidi kulipa wafanyakazi mishahara

adminleo