• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:27 PM
Wageni 10,000 kuhudhuria sherehe za kitamaduni Lodwar

Wageni 10,000 kuhudhuria sherehe za kitamaduni Lodwar

Na SAMMY LUTTA

ZAIDI ya wageni 10,000 wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kitamaduni za jamii ya Turkana zijulikanazo kama Tobong’u Lore katika ukumbi wa Ekaales mjini Lodwar, Kaunti ya Turkana zinazoanza Jumatano.

Naibu Rais Daktari William Ruto atakuwa miongoni mwa wageni maarufu ambao watajumuika na wenyeji pamoja na wageni kutoka jamii za wafugaji zinazopakana na Kaunti hiyo. Miongoni mwa jamii hizo ni Pokot, Karamajong wa Uganda, Toposa wa Sudan Kusini na Nyangatom wa Ethiopia.

Waziri wa Utalii Bw Charles Lokioto alisema jamii hizo ya wafugaji zitapata fursa ya kujumuika na kujifunza umuhimu wa uwiano kupitia utamaduni wao kimavazi, chakula, nyimbo na kadhalika.

“Serikali ya Kaunti ya Turkana itatumia fursa kuuza maeneo tofauti tofauti ya kitalii kama Ziwa Turkana, mavazi na vyakula vya kipekee na wanyamapori Turkana Kusini. Pia tunatarajia kuwarai wawekeza kuchukua fursa ili wawekeza katika Kaunti hii.” Bw Lokioto alisema.

Kamanda wa Polisi Kaunti hiyo Samuel Ndanyi aliwahakikishia wageni na wenyeji kuwa usalama utaimarishwa kwenye ukumbi wa Ekaales, mjini Lodwar kwa jumla na kwenye barabara ya Kitale – Lodwar.

Aliwaonya wajangili wenye bunduki za haramu kwamba hatua kali itachukuliwa wakionekana barabarani ili wahangaishe wanaosafiri.

You can share this post!

Kioja maafisa wa kaunti kufukua maiti na kuivua sare za kazi

Wito serikali kuu isitishe uuzaji viwanda vya miwa

adminleo