• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Polisi wanasa raia akiwa na pembe za thamani ya Sh10m

Polisi wanasa raia akiwa na pembe za thamani ya Sh10m

Na Steve Njuguna

POLISI katika Kaunti ya Nyandarua Jumatatu walimnasa mwanaume akiwa na kilo 89 za pembe za ndovu ambazo thamani yake ni Sh10 milioni katika eneo la Karampton, eneobunge la Nyandarua.

David Mwangi Ndegwa, alikamatwa wakati wa operesheni iliyoendeshwa na makachero kutoka Shirika la Kitaifa la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) kutoka Nairobi kwa ushirikiano na maafisa wa usalama.

Mwenzake alitoroka wakati wa kukamatwa kwa mwenziwe na maafisa waliojifanya wateja waliotaka kuuziwa pembe hizo.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Nyandarua Dkt Gideon Ngumi alisema makachero hao wa KWS waliandamana na polisi na kujifanya wanunuzi kabla ya washukiwa hao kuondoka kichakani wakiwa na pembe nne za ndovu.

“Pembe hizo zilinaswa na maafisa wa kutoka kituo cha polisi cha Mairo-inya kwa ushirikiano na maafisa kutoka makao makuu ya KWS baada ya kupokea habari kutoka kwa umma,” akasema Dkt Ngumi.

Afisa huyo alisema juhudi za kumsaka mshukiwa aliyetoroka zinaendelea huku mwezake akiendelea kuzuiwa na polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi ukikakamilika.

 

You can share this post!

Wito serikali kuu isitishe uuzaji viwanda vya miwa

MATHEKA: Serikali isipuuze ripoti za njaa kukumba maeneo

adminleo