• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
Kamati mpya za ubora wa bidhaa zazinduliwa

Kamati mpya za ubora wa bidhaa zazinduliwa

Na MAGDALENE WANJA

WAZALISHAJI bidhaa nchini wanatarajia bidhaa zao kufanyiwa ukaguzi wa hali ya juu ikiwa ni baada ya kubuniwa upya kwa kamati zenye jukumu la kuhakikisha ubora wa bidhaa.

Mnamo Alhamisi, kamati 50 kati ya 172 ambazo zimebuniwa upya zilizinduliwa na zinatarajiwa kuanza kazi.

Kulingana na mwenyekiti wa Baraza la Ubora la Kitaifa Bw Ken Wathome, baadhi ya mabadiliko ambayo yamefanyika ni pamoja na kuhakikisha kuwa wakuu wa kamati hizo hawana uhusiano wowote wa kibiashara katika vitengo wanavyovisimamia.

“Mabadiliko hayo ni badhi ya hatua ambazo tumezichukua ili kuhakikisha uhuru wa kamati hizo ili kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao,” alisema Bw Wathome.

Aliongeza kuwa hatua hii inasaidia katika kulitengeneza jina la KEBS ambalo limechafuka kutokana na sababu mbalimbali.

 

Mkurugenzi wa Baraza la Ubora la Kitaifa Bw Eddy Njoroge (kushoto), mwenyekiti wa Baraza la Ubora la Kitaifa Bw Ken Wathome (kati) na Mkurugenzi Mkuu wa KEBS Bw Bernard Njiraini. Picha/ Magdalene Wanja

Mkurugenzi wa baraza hilo Bw Eddy Njoroge alisema kuwa kinyume na hapo awali ambapo kamati hizi ziliendeshwa na washikadau pekee, sasa nafasi hizo ni wazi kwa wananchi wote.

“Kwa sasa tuna wanakamati kutoka vitengo mbalimbali – vya ujuzi – ambao watasaidia katika kubuni ubora wa viwango kwa bidhaa mbalimbali,” alisema Bw Njoroge.

  • Tags

You can share this post!

Kitabu chenye mada zinazohusu ICC na changamoto ya uhalifu...

MFUNGAJI BORA: Takwimu mpya zaonyesha ni Wanga na wala sio...

adminleo