• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 4:48 PM
IKO SHIDA! ‘Kikosi cha Spurs hakijafikia kiwango cha kumridhisha Pochettino’

IKO SHIDA! ‘Kikosi cha Spurs hakijafikia kiwango cha kumridhisha Pochettino’

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

KOCHA Mauricio Pochettino wa Tottenham Hotspur amekiri kwamba kikosi chake bado hakijafikia kiwango ambapo wanasoka watacheza kwa ushirikiano unaotakikana.

Kauli ya Pochettino inachochewa na ukosefu wa hamasa na msukumo kutoka kwa kikosi chake kilichopigwa na Newcastle United 1-0 wikendi iliyopita katika mechi ya EPL.

Kocha huyo ameeleza wazi kutoridhika kwake na kikosi hicho, wakati huu dirisha la uhamisho kwa timu za EPL limefungwa.

Pochettino amesema hayo wakati kuna fununu kwamba kiungo tegemeo, Christian Eriksen anapanga kuondoka.

Eriksen amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake, lakini tayari amesema yuko tayari kuondoka ili aanze maisha mapya kwingineko, huku kocha akiwa na wasiwasi kwamba huenda akaondoka kabla ya shughuli za uhamisho kumalizika Septemba 2 barani Ulaya.

Katika mechi yao ya mwishoni mwa wiki, Pochettino alimtumia Eriksen katika kipindi cha pili kama mchezaji wa akiba ambapo raia huyo wa Denmark akikumbwa na maswali mengi kutoka kwa waandishi waliomuuliza kuhusu kiwango chake duni.

“Mtu anapokuwa uwanjani, anafikiria mambo ya uwanjani. Na hata sielewi kwa nini mnaniuliza maswala haya. Tumepoteza mchezo kama timu, hivyo mtu mmoja hapaswi kulaumiwa,” alisema Eriksen.

“Ningependa mniulize maswali kama haya katikati mwa wiki, lakini sio siku ya mechi. Matokeo kama hayo hutokea katika soka, na ni juu ya kocha kutafuta mbinu mpya za kuibadilisha timu ili ishinde mechi inayofuata,” aliongeza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27.

“Kwa hakika, hatukucheza vizuri na nimekasirika sana na kiwango chetu. Tulifungwa bao la mapema, na mambo yakaanza kuwa magumu kutokea hapo. Tulibuni nafasi kadhaa lakini hatukufanikiwa kufunga mabao. Walioangalia matokeo kwa jumla, watakubali tulipoteza nafasi nyingi,’’ akasema.

Awali, kabla ya kucheza mwishoni mwa wiki, Pochettino alikuwa amekiri kwamba wachezaji pamoja na klabu kwa jumla ilikuwa ikiumizwa na hatima isiyoeleweka ya kiungo Eriksen.

Haijaeleweka iwapo nyota huyo ataendelea kuwepo Spurs, huku akiwa amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa sasa.

Ni wiki chache zilizopita klabu hiyo ilipokataa ofa nono zilizotolewa mezani kwa ajili ya kiungo huyo.

“Hali hii haifai, kwa klabu na hata kwake yeye binafsi, ingawa ni yeye atakayefanya uamuzi wa mwisho. Tutachohitaji kufanya kwa sasa ni kupunguza presha hii, na tumsihi aendelee kutusaidia,”alisema Pochettino.

You can share this post!

Mfyatukaji stadi Moraa afuzu Riadha za Dunia

Oliech adai angali mchezaji wa Gor Mahia

adminleo