• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
Balozi wa Amerika aonya kuhusu ufisadi

Balozi wa Amerika aonya kuhusu ufisadi

Na SHABAN MAKOKHA

HUENDA Kenya ikakosa kutimiza Ajenda Nne Kuu za Maendeleo ikiwa viongozi hawatakabili ufisadi, balozi wa Amerika nchini Kyle McCarter, amesema.

Balozi huyo alisema kuwa ufisadi nchini umeongezeka kiasi kikubwa, unaonekana kama makubaliano kati ya viongozi waliochaguliwa na wananchi, kwamba watawapa fedha wanazopata wanapopora mali ya umma.

“Inaonekana kuwa ni kawaida mtu kutoa hongo nchini Kenya ama kubuni mitandao ya ufisadi bila lawama zozote. Ufisadi unaonekana kama njia ya kuwawezesha viongozi kuchaguliwa na kuutumia kama mbinu ya kukwepa kukabiliwa kisheria,” alisema Bw McCarter.

Alilalama kwamba viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za ufisadi wanachaguliwa kwa urahisi kuliko wengine wenye rekodi nzuri za maendeleo.

Akizungumza Jumamosi katika Shule ya Msingi ya Mwangaza katika Kaunti Ndogo ya Lurambi, Kaunti ya Kakamega, balozi huyo alisema kuwa viongozi wanaopatikana kushiriki katika sakata za ufisadi wanapaswa kukabiliwa kisheria.

You can share this post!

Rais Kenyatta akagua miradi ya maendeleo Pwani

Orengo akosoa Rais kuhusu mswada wa fedha

adminleo