• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Waelezea wasiwasi wao kuhusu kunyanyapaliwa kwa walio na Ukimwi

Waelezea wasiwasi wao kuhusu kunyanyapaliwa kwa walio na Ukimwi

Na MAGDALENE WANJA

VIONGOZI wa kidini kutoka barani Afrika wamesisitiza kujitolea kwao katika kupigana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Wakizungumza jijini Nairobi katika hafla ya siku tatu kwa jina ‘RightBYHer’ iliyohudhuriwa na zaidi ya viongozi 60 wa kidini kutoka nchi mbalimbali, walisema kuwa wana jukumu la kuzuia unyanyapaa.

Baadhi ya viongozi wa kidini waliohudhuria ‘RightBYHer’ jijini Nairobi. Picha/ Magdalene Wanja

“Viongozi wa kidini wana ushawishi na njia za kuleta mabadiliko ili kuhakikisha kuwa wanaoishi na virusi hivyo wanaishi maisha ya kawaida,” alisema askofu mkuu wa kanisa la National Independent Church of Africa (NICA) Stephen Marete.

Hafla hiyo iliandaliwa na shirika la Faith to Action Network ambapo viongozi wa kidini waliahidi kutumia ushawishi wao kumaliza unyanyapaa kwa watu wenye virusi hivyo.

Kiongozi wa kidini wa kanisa la Seventh Day Adventist Bw Samuel Kizito alisema kuwa dini ina majukumu ya kupigana na maovu katika jamii kama vile vurugu za kijinsia (GBV).

Baadhi ya viongozi wa kidini pia waliahidi kutenga mahali ambapo waathiriwa wa maovu katika jamii na wale wenye virusi vya Ukimwi watakapokimbilia.

  • Tags

You can share this post!

ULIMBWENDE: Jinsi ya kuondoa uchafu kwenye ngozi ukitumia...

WAWERU: Aibu mabilioni kuporwa huku kukishuhudiwa uhaba...

adminleo