• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 8:55 AM
Makocha Wakenya kunolewa na Arsenal

Makocha Wakenya kunolewa na Arsenal

Na GEOFFREY ANENE

MAKOCHA Wakenya Feisal Abdi Hassan, Beldine Lilian Achieng Odemba, Susan Wanjiru Njoki na Everline Achieng Onyango wamo mbioni kufuata nyayo za Hamisi Mohamed aliyeibuka nambari moja barani Afrika na kupata mafunzo kutoka kwa klabu ya Arsenal nchini Uingereza.

Hassan, ambaye ni kocha kutoka jijini Nairobi, Odemba (kocha katika akademia ya Kariobangi Sharks), Njoki (kocha katika akademia ya Kahawa Sportive) na Onyango (kocha wa timu ya Mukuru Starlets) wako katika orodha ya makocha 16 kutoka Afrika waliochaguliwa kwa makala ya pili ya kuwania nafasi ya kuenda jijini London nchini Uingereza kunolewa na Arsenal kupitia kwa ushirikiano na kampuni ya kutoa huduma ya kifedha ya WorldRemit kupitia mpango wa Future Stars.

Jopo la majaji kutoka WorldRemit na klabu ya kukuza talanta ya Arsenal lilipitia maombi ya watu 20 walioingia nusu-fainali wakiwemo 16 kutoka barani Afrika.

Vigezo vilivyotumiwa ni kujitolea kwa kocha katika kuinua maisha ya jamii anakotoka, jinsi kazi yake imeweza kusaidia vijana katika jamii na uzito wa ombi la kocha katika kunufaisha jamii na mafunzo atakayokuwa amepata baada ya kurejea.

Makocha wote 20 waliofika nusu-fainali watazawadiwa jezi za Arsenal kwa wachezaji wanaonoa.

Kutoka orodha ya makocha 20, wanane (wanaume wanne na wanawake wanne) wataingia fainali. Hadithi zao zitachapishwa kwenye tovuti ya www.FutureStars.WorldRemit.com mwisho wa mwezi Oktoba kabla ya washindi wawili kuchaguliwa kupitia kura ya umma katika tovuti hii.

Mohamed aliibuka mshindi kwa wingi wa kura mwaka 2018 na kupata mafunzo kabla ya kurejea.

Orodha ya makocha 16 kutoka Afrika mbioni kwenye mpango wa Future Stars:

Nigeria

Uzoma Kingsley Akanador – Lagos

Ademilokun Oluwaseun David – Lagos

Chinasa Ukanda – Lagos

Towobola Grace Iyanuoluwa – Ibadan

Modupe Marilyn Jiwalde Pusmut – Jos

Kenya

Feisal Abdi Hassan – Nairobi

Beldine Lilian Achieng Odemba – Nairobi

Susan Wanjiru Njoki – Nairobi

Everline Achieng Onyango – Nairobi

Ghana

Samuel Taylor – Accra

Alhassan Iddi Manzah – Tamale-Dalun

Uganda

Bakit Isaac Agogo – Gulu

Andrew Amanya – Kabale

Nabisenke Joan – Kampala

Zimbabwe

Titus Tongesai Sanagurai – Harare

Winnet Muranganwa – Chitungwiza

You can share this post!

Mtoto mchanga apatikana katupwa kando ya lori mjini Thika

Makocha Wakenya 4 watafuta kujiongeza mafunzo Arsenal

adminleo