• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Kenya yatuama katika nafasi ya 107 Fifa

Kenya yatuama katika nafasi ya 107 Fifa

Na JOHN ASHIHUNDU

KENYA imebakia katika nafasi ya 107 duniani, kulingana na orodha ya viwango vya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) iliyotolewa Alhamisi.

Mashabiki wa soka nchini waliitarajia timu hiyo ya taifa kupiga angalau nafasi moja mbele baada ya kutoka sarae 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya kupimana nguvu.

Uganda ndiyo bora eneo la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), ikiwa hatua 27 juu ya Kenya.

Senegal waliomaliza katika nafasi ya pili katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika waliendelea kubakia kileleni barani, wakifuatiwa na Tunisia, lakini wako katika nafasi ya 20 duniani, nafasi tisa juu ya Tunisia.

Baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu katika michuano ya bara kwa ufupi kama Afcon, Nigeria wanakamata nafasi ya tatu, lakini nafasi ya 34 duniani, huku mabingwa wa Afrika Algeria wakijivunia nafasi ya 38 duniani.

Ubelgiji walihifadhi nafasi ya kwanza duniani, huku mabingwa wa dunia Ufaransa wakitosheka na nafasi ya pili, wakifuatiwa na Brazil, Uingereza na Ureno kwenye orodha ya tano bora mtawaliwa.

Timu zilizofanikiwa kupanda kwenye viwango hivyo ni Grenada waliovuka nafasi 13 wakati Nicaragua wakishuka nafasi 11 na kujipata katika nafasi ya 148.

You can share this post!

Watimkaji 14 barani ange kushiriki mbio za Safaricom Mombasa

PSG bila nyota wake wakuu yalipiza kisasi dhidi ya Real...

adminleo