Tahadhari yatolewa kuhusu kondomu mbovu
NASIBO KABALE na ANGELA OKETCH
MAMLAKA ya Kusambaza Dawa Nchini (KEMSA) imeagiza maduka kurejesha kondumu aina za ‘Sure’ kwa kutofikia kiwango cha ubora unaohitajika.
Meneja wa KEMSA Dkt John Aduda kupitia barua iliyoandikwa Septemba 12, 2019, alisema muda wa matumizi ya kondumu hizo zenye nambari 17DN754 na 17DN052 unafaa kuwa Disemba 2021 na Disemba 2022 mtawalia.
“Tunaamrisha kondumu zote aina ya Sure ambazo matumizi yake yameharamishwa zirejeshwe kwa Kemsa,” akasema Bw Aduda.
Msemaji wa masuala ya usambazaji wa dawa kwenye maabara ya Kemsa alisema wameamrishwa kuchukua hatua za kusitisha matumizi ya kondomu hizo na kampuni iliyozitengeza ya Innolatex kutoka Thailand.
Watumiaji nao wameshauriwa kuhakikisha wanaangalia jina la brandi na tarehe kwenye kondomu kuona iwapo ni zile zilizopigwa marufuku au la kabla ya kuzitumia.
Kondumu hutumika kama kinga dhidi ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa na pia upangaji wa uzazi.