• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
‘Unaponunua kipande cha ardhi fuata taratibu kisheria ili kuepuka kutapeliwa’

‘Unaponunua kipande cha ardhi fuata taratibu kisheria ili kuepuka kutapeliwa’

Na SAMMY WAWERU

KWA zaidi ya miaka 15 Hellen Jepkemoi ambaye ni mkazi wa kaunti ya Uasin-Gishu amekuwa akijaribu juu chini kutafuta hatimiliki ya kipande chake cha ardhi bila mafanikio.

Ana ekari mbili na anazosema imekuwa vigumu kupata cheti cha kumiliki ardhi hiyo.

Hata ingawa hajatapeliwa, Hellen anasema marehemu mume wake alinunua kipande hicho kabla ya mwaka wa 2000 kutoka kwa mmiliki.

“Ana kipande kikubwa cha ardhi ambacho ameuzia watu kadhaa vipande vya ardhi na hakuna aliyepata hatimiliki kufikia sasa. Hatua za kuipata zimelemazwa na ukosefu wa ushirikiano kati yetu, tulionunua na mmiliki. Kupata cheti ni gharama inayohitaji watu kushirikiana,” anaelezea.

Ameshirikisha soroveya kutoka kwa idara ya ardhi. Aidha, limewekwa vifaa vya kuonyesha mipaka.

Kisa cha mama huyo ni kimoja tu miongoni mwa wengi wanaopotia hali hiyo. Suala la ardhi na mipaka linaendelea kuwa donda ndugu maendeleo mbalimbali nchini.

Aidha, kuna baadhi ya waliopitia ukatili usiomithilika kwa sababu ya mizozo ya umiliki wa vipande vya ardhi. Si kisa kimoja au viwili, ndugu wa toka nitoke, jamaa, marafiki na jamii, wameripotiwa kujeruhiana au hata kusababisha maafa.

Idara ya ardhi ni mojawapo ya zilizosheheni utapeli, na kulingana na wataalamu na wenye tajiriba ya masuala ya mashamba wanashauri haja ya kufuata taratibu zifaazo kisheria kabla ya kununua kipande.

Iwapo umepata sehemu unayonuwia kununua, hatua ya kwanza ni kushirikisha jamaa wa mmiliki – anayeuza na majirani kujua uhalisia wa kipande cha ploti au shamba.

“Mke, watoto na majirani watakueleza ukweli na kukupa mwelekeo,” anashauri Bw James Mwangi, afisa mstaafu kutoka idara ya polisi na anayesema wakati wa huduma zake serikalini alipokea malalamishi ya mizozo ya ardhi.

Mwangi anasema wazee wa kijiji, naibu chifu na chifu wa kata pia ni asasi husika muhimu katika kujumuishwa kwenye utafiti wa uhalisia wa shamba.

“Machifu wanafahamu kata na wakazi kwa undani, hivyo basi watakushauri kununua shamba au la,” anasema.

Usikomee hapo, muhimu zaidi ni kufululiza hadi katika afisi za ardhi kufanya uchunguzi zaidi wa shamba, maarufu kama ‘land search’.

Endapo kipande cha ardhi unayopania kununua ni halali, unahimizwa kushirikisha wakili.

“Ndio wakili ni gharama, lakini ni bora kumshirikisha wakati wa kutia saini mkataba wa ununuzi,” anashauri Caroline Kanyingi, ambaye ni wakili. Rocket Casino in Australia offers good number of bonuses such as welcome packages with free spins .

Kulingana naye, endapo kipade cha ardhi ulichonunua kitaibuka kuwa na mzozo, wakili ataweza kufuatilia na hata kusaidia mnunuzi kutafuta haki kortini.

Caroline anasisitiza haja ya mnunuzi kupokezwa hatimiliki baada ya kukamilisha malipo na taratibu nyinginezo muhimu.

You can share this post!

Nyoro aomba ushirikiano kuiboresha Kiambu

Mjeledi wa FIFA wachapa, mataifa yatozwa mamilioni

adminleo