• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Jiandae kwa mvua kubwa mwezi huu

Jiandae kwa mvua kubwa mwezi huu

Na COLLINS OMULO

IDARA ya Kitaifa kuhusu Utabiri wa Hali ya Anga (KMD), imewatahadharisha Wakenya kujiandaa kwa mvua kubwa zaidi mwezi huu ikilinganishwa na mwezi uliopita huku vipindi vya mvua vikiendelea katika sehemu kadha nchini.

Mkurugenzi wa KMD, Bi Stella Aura alionya kuwa mvua hiyo, huenda ikasababisha mafuriko na maporomoko katika maeneo yaliyoathiriwa Kenya.

Alifafanua kuwa tofauti katika kiwango cha joto kwenye ziwa – almaarufu kama Indian Ocean Dipole (IOD) – kwa sasa iko katika kiwango cha juu ( +2.06) ambacho kinafaa kwa mvua kubwa nchini.

Hata hivyo, alipuuzilia mbali hofu ya kuzuka kwa El Nino akisema viwango vya El Niño–Southern Oscillation (ENSO) vimesalia wastani hadi sasa.

“Sehemu nyingi za taifa zitapokea mvua ya kadri katika mwezi huu huku Novemba kwa kawaida ikiwa upeo kwa msimu wa vuli wa msimu wa Oktoba-Novemba- Disemba (OND) msimu wa “vua fupi,” alisema Bi Aura.

Mkurugenzi huyo alisema kwamba vituo vingi vya idara ya utabiri wa hali ya anga kote nchini vilirekodi viwango vya jumla vya mvua iliyonyesha kila mwezi vilivyopiku asilimia 200 ya Jumla ya Kipindi cha Muda Mrefu cha Mwezi (LTMs) cha Oktoba.

Kituo cha Utabiri wa hali ya Anga Meru kilirekodi kiwango cha juu zaidi cha mvua cha milimita 649.1 kilichokuwa asilimia 297.1 ya LTM ya kila mwezi, Oktoba.

Mvua hiyo, alisema, iliambatana na dhoruba kali zilizosababisha mafuriko hasa katika ukanda wa Pwani, Eneo la Kati, Kusini Mashariki na sehemu kadha za Kaskazini Mashariki na kusababisha vifo na uharibifu wa mali, miundomsingi na vituo vya huduma kwa wanajamii.

“Maeneo kadha nchini yalishuhudia hali ya anga yenye unyevunyevu katika mwezi wa Oktoba. Mwanzo wa msimu wa mvua uliwadia kwa wakati ufaao katika maeneo mengi huku baadhi ya sehemu hasa kaskazini mashariki, mvua zikianza mapema kushinda ilivyotarajiwa,” alisema.

Utabiri wa Novemba uliotolewa na Idara hiyo Ijumaa iliyopita, uliashiria kwamba maeneo yanayozingira Mwambao wa Ziwa Victoria na maeneo ya Bonde la Ufa yatashuhudia mvua kubwa ambazo huenda zikazidi jumla ya kipindi kirefu, iliyopokewa katika kipindi sawia.

You can share this post!

Walinzi 4 wa sonko washtakiwa kwa kutusi polisi

Jumwa hatarini, achunguzwa kwa kumumunya mamilioni

adminleo