• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
KIBARUA KIGUMU: Arsenal inakutana na Leicester City ambayo iko katika fomu nzuri

KIBARUA KIGUMU: Arsenal inakutana na Leicester City ambayo iko katika fomu nzuri

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

LEICESTER City na Arsenal zitakutana leo Jumamosi usiku ugani King Power, katika mechi ambayo huenda ikaamua nani kati yao atamaliza katika nafasi nne za kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Vijana wa Brendan Rodgers wamekuwa katika kiwango kizuri huku wakijivunia nafasi ya tatu kwenye jedwali kutokana na ushindi mara saba katika mechi 11. Arsenal, almaarufu Gunners, wamelazimika kutosheka na nafasi ya tano, kwa tofauti ya pointi nne nyuma ya Chelsea wanaoshikilia nafasi ya nne.

Kocha wa Gunners Unai Emery, anafahamu vyema kwamba lazima vijana wake wafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya msimu huu, ili ajihakikishie nafasi ya kuendelea kukinoa kikosi hicho cha Emirates. Lakini huenda akavurugwa na Leicester ambao wamekuwa wakipata matokeo ya kuridhisha.

Inakuwa ni siku muhimu kwa Arsenal kuonyesha ari ya kuwania kumaliza miongoni mwa nne bora.

Kichapo kitapunguza matumaini yao kwa kiwango kikubwa.

Mechi hii imekuja wakati kocha Emery amemvua unahodha Grant Xhaka kufuatia tukio lake la kuonyesha hamaki dhidi ya mashabiki wa timu hiyo majuzi.

Kocha Emery amethibitisha kwamba Xhaka si nahodha wa Arsenal tena, baada ya tukio lake la kufokeana na mashabiki wa klabu hiyo alipofanyiwa mabadiliko wakicheza na Crystal Palace.

Kadhalika, kumetokea tetesi kwamba kufuatia tukio hilo, huenda klabu hiyo ikamuuza kiungo huyo katika majira ya baridi baada ya jukumu lake la unahodha kupewa Pierre-Emerick Aubameyang.

Mashabiki wengi wanaipa nafasi kubwa Leicester kuibuka na ushindi wa 2-1 kutokana na kiwango chao bora cha hivi sasa.

Arsenal wamekuwa na matatizo kweenye safu yao ya ulinzi na huenda mshambuliaji matata Jamie Verdy akwa na fursa nzuri ya kupenya ngome hiyo na kufunga mabao.

Dani Ceballos ataikosa mechi hiyo kutokana na jeraha la misuli alilopata wakicheza na Vitoria ya Ureno katika pambano la Europa League ambalo lilimalizaka kwa sare ya 1-1.

Kadhalika haijulikani iwapo Xhaka atapata nafasi kikosini baada ya kushushwa mamlaka, lakini Emery anajivunia viungo kadhaa wanaoweza kuimiliki nafasi hiyo vyema.

Aubameyanga anatarajiwa kuongoiza safu ya ushambuliaji, mbali na kuhudumu kama nahodha, huku akipata usaidizi kutoka kwa Mesut Ozil ambaye hakucheza Jumatano dhidi ya Vitoria.

Kocha Emery anatarjiwa kuanza na mabeki watatu katika juhudi za kumzuia Vardy kupenya ngome hiyo.

Kwa upande wa Leicester, kocha Rogders amethibitisha kwamba ana kikosi imara cha kuvuruga ngome hiyo.

Vikosi Leicester City (mfumo wa 4-1-4-1): Schmeichel, Pereira, Evans, Soyuncu, Chilwell, Ndidi, Perez, Tielemans, Maddison, Barnes na Vardy.

Arsenal (mfumo wa 3-4-1-2): Leno, Chambers, Sokratis, David Luiz, Tierney, Torreira, Guendouzi, Willock, Ozil, Lacazette na Aubameyang.

You can share this post!

FUNGUKA: ‘Hutaamini ninavyohifadhi kumbukumbu ya...

Kante arejea kikosini baada ya kupata nafuu

adminleo