Michezo

PRESHA URENO: Ronaldo na wenzake kikosini wanalenga kuzamisha Lithuania

November 14th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na MASHIRIKA

LISBON, Ureno

KUFUATIA kichapo cha 2-1 kutoka kwa Ukraine, kuna maana kwamba Ureno hawawezi kumaliza wa kwanza katika Kundi la B, lakini ushindi dhidi ya Lithuania leo Alhamisi usiku huenda ukawezesha kumaliza katika nafasi ya pili, iwapo Serbia watashindwa na Luxembuorg katika mechi nyingine.

Concalo Paciencia wa Eintracht Frankfurt ameitwa kikosini kujaza nafasi ya Joao Felix aliyeumia. Pia Andre Silva pia kutoka klabu ya Eintracht Frankfurt hatakuwa kikosini.

Kadhalika washambuliaji wenzake Eder na Diogo Jota wamerejea kikosini lakini Nelson Semedo amejiondoa kutokana na jeraha alilopata mwishoni mwa wiki, lakini huenda Ricardo Pereira wa Leicester City akarejea kwa mara ya kwanza tangu aichezee timu hiyo wakati wa Kombe la Dunia mwaka uliopita.

Lithuania wamepata pointi moja tu katika mechi saba na wameshindwa mara tisa katika mechi zao 11 za mchujo wa kufuzu ugenini.

Kocha wao, Valdas Urbonas amefanya mabadiliko manne kwenye kikosi chake baada ya kipa Emilijus Zubas, viungo Mantas Kuklys na Vykintas Slivka na nahodha Fedor Chernykh kurejea baada ya kupata nafuu.

Winga Arvydas Novikovas pia anatarajiwa kurejea baada ya kupigwa adhabu ya marufuku kumalizika ambapo anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Ovidijuls Verbickas anayeuguza jeraha.

Nahodha CR7

Kichapo dhidi ya Lithuania kilikuwa cha kwanza kundini katika mechi hizo za kufuzu, lakini nahodha wao, Cristiano Ronaldo yuko katika hali nzuri ya kuongoza kikosi hicho kupata ushindi.

Cristiano Ronaldo mwenyewe aliongoza timu hiyo kwa kufunga mabao manne katika ushindi wa 5-1 timu hizo zilipokutana kwa mara ya mwisho, na tayari amefunga mabao 14 kwenye kampeni hizi msimu huu.

Pointi pekee ya Lithuania ilipatikana kutokana na sare ya 1-1 dhidi ya Luxembourg, matokeo ambayo sio ya kuogofya wenyeji.

Lithuania wamefungwa mabao 19 katika mechi saba, na kufanikiwa kufunga matano pekee.

Ureno pamoja na Serbia zitajihakikishia kushiriki katika mechi za mchujo wa kufuzu hata ikiwa zitamaliza chini ya mbili bora.