• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 3:34 PM
SANAA: Safari ya Binti Afrika kimuziki

SANAA: Safari ya Binti Afrika kimuziki

Na MAGDALENE WANJA

MARAFIKI zake walizoea kumuita Binti Afrika kutokana na mtindo wake wa mavazi alipokuwa chuoni.

Bi Grace Iseme alipenda kuvalia ya mtindo wa Kiafrika hata alipokuwa akiendelea kufanya muziki wake.

Alirekodi wimbo wake wa kwanza kwa jina ‘Mo Fire’ akiwa katika kikundi cha Kreative Mynds mnamo mwaka 2000.

Kwa karibu miaka 20 sasa amekuwa akifanya muziki wa mtindo wa Swahili Dub pamoja na reggae ambao anautumia kuimba nyimbo za mapenzi.

Hata hivyo, safari yake haikuwa rahisi hapo mwanzoni.

“Nilipoanza kuimba, ilikuwa vigumu sana kwa mwanamke kubobea katika fani hii kwani changamoto zilikuwa tele kama vile kudhulumiwa kimapenzi ama kwa njia hii au njia ile,” anasema Bi Iseme.

Wimbo wake wa hivi punde unajulikana kama ‘Barua kwa Serikali’ ambao umekuwa ukichezwa sana katika vyombo vya habari hapa nchini na mataifa mengine.

Kufikia sasa ana albamu moja kwa jina ‘Sauti Inawika’ ambayo ilitoka mwaka wa 2016.

Albamu ya pili ‘Lioness Order’ anasema matarajio yake ni kwamba ataitoa kabla mwisho wa mwaka 2019.

Binti Afrika hutumbuiza katika majukwaa chungu nzima ambapo muziki wake unapendwa na mashabiki wake kutoka pembe zote hapa nchini.

“Nyimbo zangu zingine ni pamoja na ‘Mtoto Mpotevu’ nilioimba pamoja na Nonini, ‘Take it Slow’ (ambao uliteuliwa kwa Kisima Award mwaka 2009), ‘Nimekosa’ ambao nimeimba pamoja na Berry Black, ‘Access Denied’, ‘Reggae Music’ na ‘Barua kwa Serikali’,” akaongeza.

Ushauri wake kwa vijana ni kuwa kila mtu anaweza kufanya vyema katika muziki ila inachukua muda na bidii zaidi inahitajika.

You can share this post!

Green Belt wataka serikali itoe ramani kama hakikisho...

Gavana Dhadho ahimiza hatua za kiutu kusuluhisha mzozo wa...

adminleo