• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Kalonzo na Kibwana wapapurana

Kalonzo na Kibwana wapapurana

Na PIUS MAUNDU

UADUI kati ya Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka na Gavana wa Makueni, Profesa Kivutha Kilonzo ulitokota zaidi wikendi wawili hao walipotofautiana hadharani wakihudhuria mahafala katika Chuo Kikuu cha Lukenya.

Profesa Kibwana, ambaye alihutubu kwanza alimtaja Bw Musyoka kama kiongozi wa chama chake kisheria, akirejelea muafaka wa awali uliokuwa kati ya Wiper na chama cha Muungano lakini ukatupiliwa mbali baada yao kutofautiana.

Aliposimama kuhutubu, Bw Musyoka alisema Profesa Kibwana yupo chini ya himaya yake kisiasa.

“Profesa Kibwana amenirejelea kama kiongozi wa chama chake kisheria na nakubali hilo ila anafaa afahamu kwamba mimi ndiye kigogo wa chama na eneo zima la Ukambani,” alisema Bw Musyoka huku akishangiliwa na waliohudhuria hafla hiyo.

Wawili hao walikutana siku moja tu baada ya gavana huyo kumkashifu Bw Musyoka hadharani akisema hajaifaa jamii ya Wakamba kimaendeleo.

By Musyoka amekuwa akidai Profesa Kibwana pamoja na Magavana Dkt Alfred Mutua(Machakos) na Charity Ngilu (Kitui) wanapanga kumbandua kama kigogo wa siasa eneo la Ukambani na kudidimiza umaarufu wake eneo hilo.

You can share this post!

Ruto amtafute Mzee Moi amsamehe – Atwoli

ODM yashukuru Rais kuhusu BBI

adminleo