• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 10:55 AM
Raila hawezi kuaminika kisiasa – Gavana Waititu

Raila hawezi kuaminika kisiasa – Gavana Waititu

Na BERNARDINE MUTANU

GAVANA wa Kiambu Ferdinand Waititu ameelezea sababu za kutoamwamini kiongozi wa upinzani Raila Odinga, hata baada ya kukubaliana kufanya kazi na Rais Uhuru Kenyatta.

Wakati wa mahojiano katika kituo kimoja cha televisheni cha humu nchini, Waititu alisema Bw Odinga hawezi kuaminika kisiasa.

Alisema alipokuwa akifanya kazi naye kama Waziri Msaidizi wa Maji na Unyunyiziaji, aligundua kuwa alikuwa mtu ambaye hakutimiza ahadi zake.

Gavana Waititu alisema hadhalilishi mkataba wa hivi majuzi kati ya Rais Uhuru Kenyatta na waziri mkuu huyo wa zamani.

Alisema haja yake kuu kwa kutoa kauli hiyo ilikuwa ni kuwatahadharisha Wakenya kuhusu tabia na mienendo ya Bw Odinga.

Wakati huohuo, gavana huyo alizungumzia mgogoro kati yake na naibu gavana James Nyoro na kusema kuwa hali haitageuka kama ilivyofanyika Nairobi.

 

You can share this post!

Canada yaitaka Kenya itoe sababu ya kumfurusha Miguna tena

Viongozi wa Jubilee wamponda Maraga, wamsifu Matiang’i

adminleo