Chama cha Wiper chasema kinaunga kikamilifu mapendekezo ya BBI
Na WANDERI KAMAU
CHAMA cha Wiper kimesema kuwa kinaunga mkono kikamilifu ripoti ya Jopo la Maridhiano (BBI).
Kimesema kuwa msimamo wake ulidhihirishwa na kauli aliyotoa kiongozi wake Kalonzo Musyoka kwenye uzinduzi wa ripoti hiyo Jumatano katika ukumbi wa Bomas jijini Nairobi.
Ilikuwa ni siku muhimu sana kwa Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga.
Wiper hata hivyo kimesema kuwa “bado kinayapitia” mapendekezo ya ripoti hiyo.
Kikao cha Alhamisi jijini Nairobi kimehutubiwa na Bw Musyoka na mwenyekiti wa Wiper Bw Chirau Ali Mwakwere.
Kalonzo vilevile ametaka vyama vya kisasa kupewa nguvu za kuwaadhibu na kuwatoa viongozi wanaochaguliwa kwa tiketi yavyo lakini baadaye wanakiuka sheria na kanuni na kuelekea kuviasi vyama.
Kalonzo pia anapendekeza Waziri Mkuu – nafasi iliyopendekezwa na BBI – kuongezwa mamlaka kuliko ilivyo akisema ni muhimu awe angalau kiongozi wa chama chenye idadi kubwa ya wabunge, asiwe anachaguliwa pekee kutoka katika Bunge la Kitaifa na mshahara wake uwe mkubwa kuliko wa wabunge.