• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
‘Kilifi ni ngome ya magaidi na magenge ya wahalifu’

‘Kilifi ni ngome ya magaidi na magenge ya wahalifu’

Na MAUREEN ONGALA

KAUNTI ya Kilifi imetajwa kuwa maficho ya magaidi na magenge ya wahalifu ambao wamekuwa wakihangaisha wakazi wa ukanda wa Pwani.

Hii ni kulingana na shirika lisilo la serikali la kutetea amani la Kenya Community Support Centre (KECOSCE).

Akizungumza katika Chuo Kikuu cha Pwani wakati wa uzinduzi wa mpango wa usalama, mshirikishi wa miradi wa KICOSCE Hassan Kibwana alisema kuwa usalama ungali changamoto katika Kaunti ya Kilifi kutokana na ukosefu wa ushirikiano baina ya wakazi na maafisa wa usalama.

“Makundi ya uhalifu kutoka kaunti jirani yanakuja Kilifi kufanya mipango,” akasema.

Mnamo 2017, Kaunti ya Kilifi ilizindua mpango wa kukabiliana na mafunzo ya itikadi kali na ugaidi.

Miongoni mwa waliolengwa katika hamasisho hilo la kukabiliana na ugaidi ni wamiliki wa hoteli.Kaunti ya Kilifi ilikuwa ya kwanza kushambuliwa na magaidi katika Ukanda wa Pwani kwenye hoteli ya Kikambala mnamo Novemba 28, 2002.

Shambulio hilo lilihusishwa na Sheikh Abdi Rogo aliyeaminika kuwa mwanachama wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida.

Mnamo Januari 2014, aliyekuwa polisi wa akiba katika eneo la Malindi, Ahmed Asbdalla Bakhsheini, aliuawa na wahalifu walioaminika kuwa mahaidi.

You can share this post!

Nimechoshwa na huyu Ruto, Uhuru awaka

Sh500 milioni kwa atakayefichua aliko Jehad Serwan Mostafa

adminleo