• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Piano ilivyobadilisha maisha yake

Piano ilivyobadilisha maisha yake

Na MAGDALENE WANJA

Wakati Boni Fidel Odera alizaliwa, zawadi yake ya kwanza aliyopokea kutoka kwa babake ilikuwa ni piano ndogo.

Ameweka kumbukumbu hii kwenye picha ambayo iko katika muundo wa kikale wa rangi nyeupe na nyeusi.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa kazi yake ya uchezaji wa vyombo vya muziki ambayo anaifanya jijini Nairobi.

“Babangu alipenda muziki sana na nilipozaliwa, alionelea zawadi bora ni kinanda. Japokuwa sikujua kuicheza, nilijifunza nilipoendelea kukua,” anasem Odera.

Aliendelea kupenda vifaa vya muziki na ata alipokuwa akiendelea kukua, alienda kanisani ili kucheza muziki.

“Kanisa ambalo niliihudhuria liliweka vifaa vya muziki nyumbani kwetu, hii ilinifanya niwe na hamu sana ya jinsi kila moja yake ilifanya kazi,” anasema Odera.

Alikumbuka akiskiza kanada za muziki za wasanii kama vile Emachichi, Angela Chibalonza na wengine kutoka Congo kama vile Makoma.

“Kanisa hilo lilichangia sana katika kuunda maisha yangu ya baadaye.”

Katika masomo yake ya msingi na upili, alishiriki katika mashindano ya uchezaji wa vifaa vya muziki na kushinda tuzo kadhaa.

Alipokamilisha masomo yake, aliamua kufanya muziki kama kazi yake ya kila siku.

Kufikia sasa, anafanya kazi na zaidi ya bendi  tano mjini Nairobi.

Bendi hizo ni pamoja na Simply Blacque band, Sojourners reggae band, WeN music, UDU Africa, Benga Together movement na Pan – Africanism

Alisema kuwa anaupata msukumo wake kutoka kwa mpiga ngoma Henry Saha kutoka Pwani.

You can share this post!

Ni upuuzi kusema makontena yanatumika kwa uuzaji wa...

Ashtakiwa kulaghai wawekezaji Sh19m

adminleo