Roma yaingia nusu fainali baada ya kuangusha jabali Barcelona
Na CHRIS ADUNGO
KWA mashabiki wengi, ilikuwa ndoto kwa AS Roma ya Italia kuwazia timu hiyo kuibandua Barcelona na kuingia nusu fainali ya UEFA Klabu Bingwa Ulaya.
Lakini timu hiyo ilijikaza kiume ikijua kuwa tayari ilikuwa na bao la ugenini na kuizaba Barca 3-0 nyumbani katika uwanja wa Stadio Olimpio na kufanya matokeo ya kumla kuwa 4-0. Bao la ugenini iliwahakikishia nafasi kwenye nusu fainali.
Roma ilianza kuimumunya Barca katika dakika ya sita wakati mshambuliaji Edin Dzeko alipokea pasi safi ndefu kutoka kwa kiungo mwenye uzoefu mkubwa Daniele de Rossi na kuitia ndani ya neti na Marc-Andre ter Stegen akiduwaa.
De Rossi aliongeza la pili kupitia mkwaju w apenalti baada ya Dzeko kuangushwa kwa kisanduku cha Barca mapema katika kipindi cha pili na kulazimisha matokeo ya jumla kuwa 4-3.
Roma ilichanja kona ambayo Kostas Manolas aliifunga kwa kichwa na kuhakikisha kuwa Barca imeaga kipute hicho, ijaribu tena msimu ujao.
Mashabiki wengi walitamauka jinsi nyota Lionel Messi alishindwa kuisaidia timu yake kufika nusu fainali ikiwa tayari na mabao manne.