• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Serikali yakanusha madai kwamba imeshindwa kuingiza ARVs nchini

Serikali yakanusha madai kwamba imeshindwa kuingiza ARVs nchini

Na MAGDALENE WANJA

SERIKALI imekanusha madai kwamba dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) zilizokuwa zinaelekezwa Kenya zilipelekwa katika mataifa ya Afrika Magharibi baada ya serikali kushindwa kulipia kodi.

Hii inajiri juma moja baada ya madai hayo ambayo yaliibua hisisa kali kutoka kwa Wakenya hasa mitandaoni.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa akaunti yake katika mtandao wa Twitter, Wizara ya Afya ilijitetea na kudai kwamba aina hizo za dawa kwa kawaida huwa hazitozwi kodi yoyote ili kuingia nchini.

“Tungependa kuweka wazi kwamba dawa zinazonunuliwa kupitia PEPFAR na Global Fund hazitozwi kodi yoyote,” linasema chapisho la wizara.

Wakenya walilaumu serikali kwa kukosa umakini na kutokuwa na juhudi katika vita dhidi Ukimwi ambao kwa miongo kadhaa sasa umebakia tishio kwa vizazi.

“KEMSA ni kiungo cha Wizara ya Afya ambacho kinashughulika na ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa dawa,” ilisoma taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa ununuzi wa dawa zitakazosambazwa mwaka huu 2020 tayari umeanza.

  • Tags

You can share this post!

Gor, Tusker wajikita kileleni Homeboyz, Ulinzi wakipaa

Watumiaji mitandao ya kijamii wakashifu hatua ya Miguna...

adminleo