• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 5:29 PM
Jinsi kuvuta sigara kiholela kunavyoweza kuingiza mtumiaji matatani

Jinsi kuvuta sigara kiholela kunavyoweza kuingiza mtumiaji matatani

Na MAGDALENE WANJA

KUVUTA sigara katika maeneo ambayo ni marufuku kunaweza kukufanya ufungwe kwa miezi sita korokoroni au kutozwa faini ya Sh50,000.

Hii ni baada ya uamuzi wa mahakama ya juu zaidi ambao umeidhinisha kutekelezwa kwa sheria ya Tobacco Control Regulations 2014.

Kulingana na waziri wa Afya Sicily Kariuki, uamuzi huo ambao ulifanywa zaidi ya mwezi mmoja uliopita ni hatua kubwa katika kuzuia maradhi na vifo vinavyosababishwa na uvutaji sigara.

“Uamuzi huo utasaidia sana katika utekelezaji wa sheria ambayo imekuwa kwa miaka mingi na itawezesha kuadhibu watu wanaovunja sheria hiyo,” alisema Bi Kariuki.

Baadhi ya maeneo marufuku kwa uvutaji wa sigara ni kama vile magari ya umma, vyumba vya kuishi, ofisini, kazini, mikahawa na hotelini, vituo vya garimoshi na maeneo ya mapokezi.

Mahakama ya juu mnamo Novemba 26, 2019, iliamuru sheria hiyo kutekelezwa mara moja.

Kulingana na sheria hiyo, uvutaji sigara unaweza kusababisha maradhi mabaya na hata kifo.

You can share this post!

Ataka idhini aoe mke wa nduguye

Miguna anajikaanga mwenyewe – Wadadisi

adminleo