• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Yaibuka ukafiri husukuma vijana kuua wazee

Yaibuka ukafiri husukuma vijana kuua wazee

Na CHARLES LWANGA

UKAFIRI na ukosefu wa msingi mwema wa kidini umedaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wazee kwa shutuma za uchawi na uzorotaji wa maadili mema kwa vijana eneo la Ganze, Kaunti ya Kilifi.

Kufikia sasa, polisi wanasema kuwa wazee wapatao 100 wameuawa kwa kuvamiwa na umma katika kaunti ya Kilifi kwa kipindi cha miaka miwili pekee..

Uchunguzi umebaini kuwa mauaji hayo wakati mwingi hutokana na mizozo za kifamilia na tamaa ya kurithi mali na ardhi za wazee hao.

Kasisi Ben Maruko wa kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) alisema wanakamilisha wiki mbili za kueneza injili nyumba kwa nyumba ili kuelimisha jamii na mafundisho ya Kikristo ili kukomesha mauaji.

Kwenye kikao cha wanahabari Ganze alipoandamana na waumini wake, alisema visa vya mauaji ya wazee ia husababishwa na matumizi ya dawa za kulevya baini ya vijana.

“Katika harakati za kutembelea wakazi makwao, tulipata kuwa wengi wao hasa vijana hawashiriki makanisani na msikitini ili wapokee mafunzo mema ya kidini na hivyo kusababisha ongezeko la visa vya wanafunzi kula ‘mogokaa’ na kunywa pombe kiholelaholea,” alisema.

Bw Maruko aliwahimiza wakazi wawe na utu na waheshimu maisha ya binadamu kama mbinu moja wapo ya kukabiliana na janga la mauwaji ya wazee kwa madai ya kufanya ushirikina.

Tayari, wakazi wa Ganze wamefungua kituo cha Kaya Godhoma cha kuwaokoa wazee waliokuwa wamepangiwa kuuliwa kwa shutuma za uchawi eneo la Mrima wa Ndege ambapo wanaishi na kupokea mawaidha ya kisaikolojia.

You can share this post!

Kilabu cha densi za uchi chafungwa

Kisasi dhidi ya Amerika ni lazima – Iran

adminleo