• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
Msomi Prof Euphrase Kezilahabi aombolezwa

Msomi Prof Euphrase Kezilahabi aombolezwa

Na WANDERI KAMAU

MWANDISHI maarufu wa Fasihi ya Kiswahili, Profesa Euphrase Kezilahabi, alifariki Alhamisi akiwa na umri wa miaka 76.

Kwa mujibu wa Bw Hezekiel Gikambi, ambaye ni mwandani wake wa karibu, msomi huyo alifariki jana nyumbani kwake jijini Dar es Salaam baada ya kukumbwa na kiharusi.

“Alipatwa na kiharusi mnamo 2018. Alipoteza fahamu na amekuwa akipata matibabu,” akasema Bw Gikambi kwenye mahojioano na ‘Taifa Leo.’

Baadhi ya kazi zake ni riwaya kama ‘Rosa Mistika,’ ‘Nagona’, ‘Mzingile,’ ‘Kichwamaji’ kati ya kazi zingine. Vile vile ameandika tamthilia na hadithi fupi.

Miongoni mwa wasomi waliommiminia sifa ni Prof Ken Walibora, Bw Bitugi Matundura, Bw Hassan Muchai kati ya wengine.

Prof Walibora alisifu sana kazi zake, akisema kwamba zilikuwa na upekee mkubwa uliokuwa na athari kubwa katika jamii.

“Ni mwandishi wa kipekee ambaye kazi zake zimetasfiriwa na kuhakikiwa sana kutokana na uzito wa kimawazo,” akasema Prof Walibora.

Amefunza vyuo mbalimbali duniani, kikiwemo Chuo Kikuu cha Botswana, nchini Botswana.

Msomi huyo alizaliwa mnamo Aprili 13, 1944 katika kisiwa cha Ukerewe nchini Tanzania.

Alisomea katika vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Winsconsin-Madison, nchini Amerika, alikopata shahada ya uzamifu (PhD).

You can share this post!

Wazee walaani serikali kumtesa Miguna

Malumbano yachacha vikao vya BBI vikianza

adminleo