• Nairobi
  • Last Updated March 18th, 2024 8:55 PM
FUNGUKA: ‘Nawapandisha mzuka baharini…’

FUNGUKA: ‘Nawapandisha mzuka baharini…’

Na PAULINE ONGAJI

RITA ni binti wa miaka 45.

Yeye ni mkazi wa Pwani ya Kenya na anaendesha biashara zake kwenye ufuo wa Bahari Hindi.

Mazingira hayo yamemsukuma kuiga maisha ya ufuoni sawa na madume wanaofahamika kama ‘beach boys’, kuuzia watalii bidhaa na kuwaelekeza katika sehemu hii.

Lakini mbali na hayo, pia ameongeza huduma isiyo ya kawaida katika kazi yake. Kwa ufupi, Rita ni kahaba na amenoa ustadi wake katika masuala ya mahaba ambapo anatoa huduma zake mle mle baharini.

Wateja wake ni watalii na wanaume wengine wanaozuru sehemu hii ambapo anawahudumia mle mle baharini badala ya chumbani.

“Nilianza maisha haya nikiwa mdogo na tangu wakati huo nimekuwa nikiendeleza kazi yangu baharini. Kazi yangu inahusisha kushiriki mahaba na madume hasa wa kitalii ndani ya bahari.

Ni kazi ambayo nimebobea kwayo kiasi kwamba naweza kumhudumia jamaa hata mbele ya mkewe, bila yeye kujua. Mwanamume anaweza wasili na mkewe ambapo tutakonyezeana jicho na pamoja tunamdanganya mwanamke kwamba namfunza mbinu mpya za kuogelea na muda si muda tunamhepa na kwenda mbali kidogo baharini kumalizia shughuli.

Kuna wakati ambapo twaweza maliza kiu yetu hapo hapo machoni mwa mkewe na sababu kuwa ni majini, hakuna hata mmoja ambaye amewahi gundua kinachoendelea.

Hii imenifanya kusakwa sio tu na watalii wa kizungu bali pia wanaume wengine kutoka humu nchini wanaozuru ufuoni wakiwa likizoni, ambapo wengi wao hunipigia simu na kupanga kupokea huduma hizi pindi wanapofika mjini.

Kutokana na kazi yangu nzuri, kuna baadhi ya madume wanaofadhili maisha yangu ghali.

Kuna mmoja ambaye ameninulia jumba katika eneo la Nyali, mmoja ameninunulia gari la kifahari na mwingine ananilipia karo ya chuo kikuu.

Isitoshe, kila wakati nikiishiwa na pesa, nawapigia simu tu na muda si muda napokea senti katika akaunti yangu.

Siogopi kuambukizwa maradhi ya zinaa licha ya kuwa kila ninapojihusisha katika shughuli hizi situmii kinga.

Hii ni ajira kama zingine ambapo kabla ya kuondoka kwenda kazini mimi humuomba Mungu anilinde.

Nimenoa makali haya kiasi kuwa iwapo siko kazini, nafanya mazoezi kuhakikisha kuwa mwili wangu unapata nguvu tayari kwa huduma inayofuatia.

Hata natarajia kuwa mke wa mtu kwani nina mchumba aliyeniposa rasmi ambapo pamoja na jamaa zake, wanafahamu ninachofanya na kutokana na sababu kuwa kazi ni kazi, hakuna anayelalama.

Nimeweza kununua majumba kadha na vipande vya ardhi ambapo tayari najenga nyumba za watu kulipia kodi. Pia nina magari na biashara zingine; vyote kutokana na kazi ninayofanya, na hivyo sijutii lolote”.

You can share this post!

Baharia afariki, wawili waokolewa baada ya mashua kuzama...

MAPISHI: Jinsi ya kuandaa mbuzi ulaya

adminleo