• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Teknolojia ya lugha ina umuhimu gani kwa Kiswahili katika Karne ya 21?

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Teknolojia ya lugha ina umuhimu gani kwa Kiswahili katika Karne ya 21?

Na MARY WANGARI

NINI umuhimu wa teknolojia ya lugha kwa Kiswahili katika karne hii?

Teknolojia ya lugha ni suala la kisasa katika karne hii ya utandawazi na mitandao ya kijamii.

Kila nyanja ya maisha ya binadamu iwe kijamii, kisiasa au kiuchumu inatumia inategemea pakubwa teknolojia ya lugha.

Hivyo basi kama wadau wa Kiswahili hatuna budi kukumbatia teknolojia ili kukuza kuendeleza na kustawisha lugha ya Kiswahili.

Kiswahili katika mawasiliano na biashara kiteknolojia

Kama anavyobainisha Mabeya (2009), tayari lugha ya Kiswahili imepiga hatua muhimu katika ulingo wa teknolojia huku matumizi yake yakishuhudiwa katika mitambo ya benki (ATM), kampuni za simu na kampuni za huduma za kompyuta kama Microsoft East Africa, Linux, Google.

Ufanisi huu katika kujumuisha Kiswahili katika teknolojia ya lugha umetokana na juhudi na ushirikiano wa wadau wa Kiswahili katika bara la Afrika na mataifa ya ulaya.

Kiswahili kimefanyika lugha rasmi nje ya mipaka ya kitaifa

Taasisi ya Lugha za Kiafrika – ACALAN yenye makao yake mjini Bamako nchini Mali, mnamo 2011, chini ya Muungano wa Afrika (AU) ilikifanya rasmi Kiswahili kuwa lugha ya mazungumzo nje ya mipaka ya kitaifa na kuunda tume kwa jina 4KVCBLC) iliyo na wadau kutoka kila taifa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hatua hii muhimu barani Afrika Mashariki na Afrika ya Kati, ilijiri miaka kadhaa baada ya AU kuitunukia Kiswahili heshima kuu kwa kuifanya lugha pekee rasmi ya Kiafrika katika muungano wa AU.

Uundaji wa Kongoo

Ni kutokana na shinikizo la kutumia teknolojia ya lugha katika karne hii ambapo taasisi husika imeanzisha rasmi mchakato wa kuunda kongoo kubwa zaidi ya lugha ya Kiswahili.

Kama anavyoeleza Matsinhe, 2015, haya yalifanikishwa kupitia utafiti kidijitali ikiwemo warsha mahususi iliyoandaliwa kwa lengo la kuwafundisha wanaisimu kongoo na wataalamu wa Kiswahili kuhusu masuala ya uundaji wa kongoo mnamo 2015.

Kwa hakika, juhudi zote hizi zinaashiria mwamko mpya katika mtazamo unaohusu kongoo ikiwemo kushirikisha zaidi teknolojia ya lugha katika utafiti wa lugha ya Kiswahili badala ya kutegemea mbinu za kimapokeo kama vile ung’amuzi katika utafiti.

Aidha, pana haja ya kuendeleza na kuboresha utafiti uliofanywa na watafiti waliotangulia kwa kutumia mbinu za kijarabati na kisayansi na kukusanya data thabiti zinazoweza kutegemewa katika kizazi hiki.

Kiswahili katika kuendeleza utafiti kidijitali

Aidha, pana haja ya kuendeleza na kuboresha utafiti uliofanywa na watafiti waliotangulia kwa kutumia mbinu za kijarabati na kisayansi na kukusanya data thabiti zinazoweza kutegemewa katika kizazi hiki.

Kama anavyoeleza Hurskainen (2008) watafiti waliotangulia kuhusu teknolojia ya lugha waliona kuwa matumizi ya kompyuta katika kuchambua lugha za Kiafrika yataharakisha mchakato wa uchambuzi huo.

Aidha, matumizi ya teknolojia yangefaidi utafiti pakubwa kupitia uundaji wa mbinu za kikompyuta kama vile mbinu za kusahihisha lugha kama vile vitathmini tahajia, mbinu za kutunga kamusi na kadhalika zinazoweza kutumika kutafuta data mbalimbali katika kongoo kwa ufasaha mkubwa, hoja inayoungwa mkono na Sewangi 2000, 2001, Hurskainen 2003 na Muhirwe 2007.

Bila shaka teknolojia ya lugha na matumizi ya teknolojia katika utafiti ina manufaa tele kuliko mbinu za kubahatisha dhana kwa kutumia data chache za lugha.

Kuchanganua kongoo-matini inayosheheni idadi ya mamilioni ya maneno kwa kutumia programu ya kompyuta kwa muda mfupi, kunaibua data za kuaminika zaidi ikilinganishwa na kuchambua sampuli ndogo ya data ya wazungumzaji yenye maneno machache. Teknolojia ya lugha hivyo basi inafaa hata zaidi kwa kuwa inadhihirisha kuwa na manufaa na yenye kasi zaidi hivyo kuweza kuwa ya kutegemewa zaidi.

Nafasi ya binadamu katika Kiswahili kiteknolojia

Hata hivyo, ni muhimu kuelewa kuwa, japo teknolojia ni muhimu katika lugha, utafiti na hata tafsiri, hatuwezi kupuuza nafasi ya binadamu katika ukuzaji na maendeleo ya lugha.

Ni muhimu kuelewa kuwa kuna nafasi ya binadamu katika michakato yote hii na hivyo hatutarajii kuwa kompyuta hufanya kila kitu yenyewe kama anavyofafanua Hurskainen (2009). Umuhimu mwingine wa teknolojia ya lugha katika Kiswahili ni kuendeleza mradi wa SALAMA na programu zake mbalimbali katika mchakato ulioanzishwa na watafuti waliotangulia.

Kiswahili kiteknolojia katika uundaji wa istilahi: Hii ni pamoja na kuendeleza mchakato wa kuunda istilahi katika mradi wa Microsoft-East Africa kama anavyoafanua Mabeya (2009) kwamba lugha ya Kiswahili imefikia kiwango cha kwenda sambamba na teknolojia ibuka ya tarakilishi na hivyo inafaa kufanyiwa utafiti zaidi.

Aidha, mwanaisimu huyu anahoji kwamba pana haja ya kuangalia miradi inayoweza kusaidia katika utafiti wa Kiswahili kiteknolojia akitaja mradi wa Microsoft East Africa kama mkakati tu wa biashara ya kimataifa ya kuuza bidhaa ororo au programu zake na wala si juhudi zilizolenga kukuza utafiti wa Kiswahili.

Hivyo basi, pana haja ya wadau wa Kiswahili kuanza tafiti zinazolenga na kutilia maanani kukuza lugha ya Kiswahili kiteknolojia.

 

[email protected]

Marejeo

Allwood, J., Mfusi.M, na Hendrikse, R (Wah) (2005), Guidelines for Developing Spoken Language Corpora. Pretoria, 2005 Southern African Language Corpora Series (Potchefstroom) Volume 1 (Potchefstroom) Juzuu 1.

Katamba, F. and Stonham J., (2006), Morphology.(2nd Edition) Palgrave Macmillan. Hampshire.

McEnery, T na Hardie, A. (2012) Corpus Linguistics: Method, Theory and Practice Cambridge. Cambridge University Press.

You can share this post!

Wazee kukagua ‘muratina’ ya kutumika katika...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Msambao wa Kiswahili Uganda...

adminleo