• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 10:55 AM
Nzige sasa wasababisha uharibifu Embu

Nzige sasa wasababisha uharibifu Embu

GEORGE MUNENE na BENSON MATHEKA

WAKAZI wa Kaunti ya Embu wamekumbwa na wasiwasi baada ya nzige kuvamia mashamba yao.

Wadudu hao waharibifu walitua katika vijiji vya Kiambere na Mutuavale na inaaminika walitoka Kaunti ya Kitui.

Ripoti zilisema walivamia mashamba ya mawele na malisho na kusababisha uharibifu mkubwa.

Naibu kamishna wa Mbeere Kusini, Charles Igiha alisema waliingia Embu kupitia Isako karibu na mpaka wa kaunti hiyo na Kitui.

Bw Igiha alisema Wizara ya Kilimo imefahamishwa kuhusu uvamizi huo.

Kaunti nyingine zilizoathiriwa na wadudu hao ni Isiolo, Samburu, Wajir, Garissa, Marsabit, Laikipia, Mandera, Kitui, Baringo na Turkana.

You can share this post!

AKILIMALI: Alianza ukulima akiwa mwanafunzi na sasa amepiga...

Umoja wa Nasa ‘wafufuka’ katika mkutano wa BBI...

adminleo