• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:47 AM
Serikali yaajiri mtaalamu kutathmini uharibifu wa nzige

Serikali yaajiri mtaalamu kutathmini uharibifu wa nzige

NA GEORGE MUNENE

WAZIRI wa Kilimo Peter Munya Jumapili alitangaza kwamba serikali imeajiri mshauri maalum kwa lengo la kutathmini uharibifu uliosababishwa na nzige kote nchini.

Waziri huyo aliyekumbana ana kwa ana na mamilioni ya nzige ambao wamevamia eneo kame la Mbeere, Kaunti ya Embu alifichua kwamba mtaalam huyo anatarajiwa kubaini hasara ambayo wahasiriwa wamepata ndipo wapewe wasaidiwe.

“Tungependa kujua kiwango cha mimea iliyoharibiwa ili tusake namna na mbinu za kuwasaidia,” alieleza wakazi katika Kijiji cha Karambari, eneobunge la Mbeere Kaskazini baada ya kuzuru eneo hilo.

Akiandamana na Mbunge Muriuki Njagagua, waziri huyo alisema mshauri huyo na kundi la wataalam hivi karibuni watatumwa katika kaunti zilizoathiriwa ili kutekeleza shughuli hiyo upesi.

Hata hivyo, aliwahakikishia Wakenya kwamba serikali ilikuwa imejitolea kuangamiza wadudu hao wanaosababisha uharibifu mashambani.

“Tuna kemikali na vifaa vya kutosha kupambana na nzige hao na watu hawafai kuendelea kuogopa,” alisema.

Alikiri kwamba wadudu hao ni hatari lakini akawaeleza wakazi kwamba serikali iko na uwezo wa kukabiliana nao.

Alisema kwamba kundi jipya la nzige waliokuwa wametua Embu ni wale waliokomaa na wameanza kutega mayai.

You can share this post!

MATHEKA: Mikutano ya wanasiasa kuhusu BBI haifaidi raia

Echesa asukuma Ruto kona mbaya

adminleo