• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
ERC kuwakamata wanaouza mafuta yanayoharibu injini za magari

ERC kuwakamata wanaouza mafuta yanayoharibu injini za magari

Na BERNARDINE MUTANU

Tume ya Kudhibiti Kawi nchini (ERC) imeanza msako wa kuwakamata madereva wanaosafirisha mafuta chafu.

Shirika hilo litapiga marufuku leseni za madereva wa malori hayo. Kabla ya kuanzisha operesheni hiyo, tume hiyo ilitoa onyo kali kwa madereva wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

Kulingana na ERC, mafuta ya aina hiyo uharibu injini na kuwapa hasara kuu waendeshaji magari na kuathiri shughuli za uchukuzi.

Baadhi ya madereva wengi wanaolengwa ni wale wanouza mafuta ambayo ni ya masoko mengine humu nchini, wanaopatikana wakiwa wameegesha malori yao kwa vituo ambavyo havina leseni, na wale wanaodhibitishwa kuendesha magari vibaya wanapochukua bidhaa hiyo.

Kulingana na ERC, maeneo ya Magharibi na Mlima Kenya ndio mabaya zaidi katika kuchanganya  na kuchafua mafuta.

Wiki jana, madereva watano walikamatwa wakiwa na makosa tofauti na tayari wamepigwa marufu kusafirisha bidhaa hiyo.

Kulingana na Mkurugenzi wa ERC Pavel Oimeke, katika muda wa miezi mitatu kufikiwa Machi 31, 2018, maeneo 20 kote nchini yalipatikana kuuza mafuta chafu.

Maeneo hayo ni  Downer’s (Kasarani), Perazim na Imperial (Longonot), Mzee wa Nyama (Nakuru), BM (Meru), Jama (Kirinyaga), Rice Enterprises (Meru).

Pia ilipata maeneo yasiyo na leseni Chulaimbo karibu na soko la Lela (Kisumu) na Bukembe (Bungoma).

You can share this post!

Matrilioni ya pesa sasa hutumwa kwa simu

Kushuka kwa bei ya Petroli kwawafaa wenye magari

adminleo