Mataifa ya kigeni yanavyokabiliana na coronavirus
NA MWANDISHI WETU
Amerika
Rais Donald Trump ametangaza kundi la kuongoza mapambano dhidi ya homa hiyo likiongozwa na Makamu Rais Mike Pence.
Korea Kusini
Serikali ya Korea Kusini imeanzisha huduma ya simu inayowasaidia wote wanaoingia nchini humo kujipima wenyewe na kupiga ripoti iwapo wana dalili zozote za virusi hivyo.
Pia mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Korea Kusini na Amerika yamefutiliwa mbali.
Korea Kaskazini
Vyombo vya habari vya serikali pamoja na vipaza sauti katika maeneo ya umma vimekuwa vikitoa habari kila siku kuhusu coronavirus na kutaka raia wote kutii maagizo.
Pia wageni wote wanaoingia nchini humo kutoka nchi za kigeni wanatengwa kwa siku 30 huku maafisa wa afya wakizuru watu manyumbani kuwafanyia ukaguzi.
Italia
Katika miji 11 ambayo imeripoti visa vya coronavirus, wakazi wapatao 55,000 wamewekewa marufuku ya kutotoka ama kuingia katika miji hiyo.
Uingereza
Walimu na wanafunzi waliokuwa wamerudi Uingereza kutoka safarini Italia watakiwa kukaa manyumbani hadi ithibitishwe hawajaambukizwa virusi hivyo.
Mashirika ya ndege yakatiza safari nchini Italia ambayo kufikia jana ilikuwa imeripoti visa 400 vya maradhi hayo.
Ireland Kaskazini
Mashindano ya raga ya mataifa sita iliyokuwa imepangwa kuchezwa Machi 7 kati ya Ireland Kaskazini na Italia mjini Dublin yaahirishwa.
Japan
Waziri Mkuu Sinzo Abe aagiza kufutwa kwa hafla zote za michezo na maonyesho kwa wiki mbili.
Iran
Iran yafunga kwa muda shule, vyuo na vituo vya kitamaduni.
Saudi Arabia
Saudi Arabia imesimamisha ziara zote katika maeneo matakatifu kwa Waislamu ya Mecca, Kaaba na Msikiti wa Nabii Muhammad mjini Medina.
Kampuni ya Facebook imepiga marufuku matangazo yanayoahidi kutibu coronavirus ama kusambaza hofu.
Matangazo hayo ni pamoja na ya vitambaa vya kufunika mapua na midomo yanayoahidi kuzuia maambukizi kwa asilimia 100.