Kimataifa

Kimbunga chaua wawili, chaharibu nyumba 40

March 3rd, 2020 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA Na MARY WANGARI

KIMBUNGA kilizuka Nashville, Tennessee mnamo Jumanne, Februari 3 alfajiri na kuwaua watu wasiopungua wawili, kuharibu takriban majengo 40 na kuwaacha maelfu ya watu bila stima.

Maafisa wa Polisi wa Metro Nashville waliripoti vifo hivyo viwili katika eneo la Nashville Mashariki.

Idara ya Zima moto Nashville ilisema ilikuwa ikijibu ripoti kuhusu majengo yapatao 40 yaliyoporomoka mjini Nashville.

Idara ya polisi katika eneo la Mlima Juliet mashariki mwa Nashville iliripoti kuhusu nyumba kadha zilizoharibiwa na watu kujeruhiwa.

“Kuna mifereji ya gesi inayovuja, laini za umeme zilizo chini na maafisa kadhaa wa kukabiliana na dharura wanashughulikia wale waliojeruhiwa,” idara ya polisi ya Mt. Juliet ilisema.

Tennessee ni miongoni mwa maeneo 14 Amerika yatakayopiga kura Jumanne katika kinyang’anyiro cha kumchagua mteule wa Demokrasia atakayesimama dhidi ya Rais Donald Trump mnamo Novemba.

Kituo cha Shughuli za Dharura Nashville kilitangaza kwamba kilikuwa kimefungua kituo cha dharura chenye maji ya mifereji katika soko la wakulima kuwasaidia raia walioachwa bila makao.

Shule zitafunguliwa mnamo Jumanne kutokana na uharibifu wa kimbunga hicho kote Nashville, na Metro Schools, alisema kwamba vituo vya uchaguzi katika shule hizo vitafunguliwa.

Nashville Electric, kituo cha umma mjini humo kilisema kwamba kulikuwa na wateja zaidi ya 44,000 bila stima alfajiri huku uharibifu ukiripotiwa kuhusu vituo vinne, laini 15 za usambazaji na vikingi kadhaa na laini za umeme.

Uwanja wa Ndege wa John C. Tune Airport (JWN), uliopo maili 8 kutoka sehemu ya chini ya Nashville, “ulipata uharibifu mkubwa ” kutokana na hali mbaya ya anga na majumba kadha ya ndege yameharibiwa, uwanja huo wa ndege ulisema kwenye tovuti yake.

Watu kadha walijitosa kwenye mtandao wa Twitter kusema hawakuwa na umeme eneo hilp.

Baadhi walichapishas video za radi kwenye mawingu.