• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Wanafunzi 98 Mukuru waokolewa na kupewa ufadhili wa masomo

Wanafunzi 98 Mukuru waokolewa na kupewa ufadhili wa masomo

Na SAMMY KIMATU

WANAFUNZI 98 katika mitaa ya mabanda ya Mukuru katika tarafa ya South B wamekuwa nyumbani baada ya kukosa karo ya sekondari.

Aidha, kila shule katika kaunti ndogo ya Makadara, kaunti ya Nairobi zimeagizwa kupandisha bendera ya taifa la Kenya ili kuonyesha uzalendo.

Haya yalinenwa Ijumaa na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ndogo ya Makadara, Bw James Koigi.

Bw Koigi alikuwa akiongoza hafla ya kukutana na wazazi na watoto waliokosa shule ili azungumze na kuona jinsi wanafunzi watakavyoendelea kusoma.

Shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mukuru Promotion Centre (MPC)

Mwenyeji wake, Mtawa Mary Killeen, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa MPC, alisema mradi wake utafadhili masomo ya wanafunzi hao.

Aliongeza kwamba atashirikiana na serikali kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayebakia nyumbani bora amatoka katika mitaa ya mabanda ya Mukuru mkwenye eneo la South B.

Alisema katika Shule ya Upili ya St Michael kulikuwa na nafasi chache zitakazopatiwa baadhi ya watoto kisha walliobakia wasomee shule zingine za serikali.

Kunazo shule mbili za upili za kibinafsi watoto husoma na kulala nyumbani katika eneo la South B ambazo ni St Michael na Brightstar Secondary.

“Nia ni kuona kila mtoto katika mtaa wa mabanda wa Mukuru anasoma. Tunalenga kuona mtoto aliye chini kimasomo ana cheti cha kidato cha nne,” mtawa Mary akasema.

Bw Koigi alisema ni shule mbili za serikali katika Makadara sio za kulala ambazo ni Makongeni na Star of hope.

Vilevile, Mtawa Mary aliwasahauri wazazi kuwatafutia wanao nafasi katika vyuo vya anwai ili wapate kujiunga na taaluma za kiufundi mbalimbali.

Viwango vya umaskini katika mitaa ya mabanda ya Mukuru viko juu ndiposa idadi ya watoto wasiokuwa shuleni inapanda kila uchao.

“Utakuta wazazi wanapigana na kuwachana. Wamama wengine wanauza pombe na watoto wanashuhudoia mama akaileta mwanamume mwingine kwa nyumba huku wanawake wengi wakifanya kazi za sulubu mitaani,” akanena Mtawa Mary.

Kutokana na sheria kali ya serikali kwamba kila mtoto ni lazima awe shuleni, baadhi ya wazazi walikiri kwamba huficha kueleza wana watoto nyumbani ambao hawasomi baada ya kukosa karo.

Wazazi wengine walisema nao hawana pesa za kugharimia sare za shule.

Akiwapa moyo na ushauri wake, Bw Koigi alisema wazazi wakikosa pesa za karo, wavalishe watoto sare walizokuwa wakitumia wakiwa katika shule za msingi.

You can share this post!

Ruto awasili Rongai kwa mazishi ya Kenei

Mashabiki wa Harambee Stars kuingia mechi ya Comoros bila...

adminleo