Akaunti za Keroche zafungwa kwa kudaiwa Sh9b na KRA
Na Mary Wangari
MAMIA ya wafanyikazi wa kampuni ya pombe ya Keroche Breweries, wamo katika hatari ya kufutwa kazi baada ya Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) kuiweka katika hatari ya kufungwa.
Hapo , KRA ilifunga akaunti za Keroche Breweries, siku mbili tu baada ya mahakama kuagiza kampuni hiyo ilipe ushuru wa Sh9 bilioni.
Haraka hiyo ya kufunga akaunti inazua maswali kuhusu nia ya serikali kuhusu Keroche Breweries.
Kampuni hiyo ni moja ya kujivuniwa na Wakenya kutokana na juhudi za mwekezaji Tabitha Karanja ambaye alisimama kidete kumaliza uthibiti wa sekta ya bia ulioshikiliwa na kampuni moja pekee.
Kampuni hiyo inekuwa na mzozo na KRA uliodumu miaka mitano.
Masaibu ya Keroche yataongeza idadi ya Wakenya wasio na kazi na kuzamisha ndoto za raia walio na bidii kufanikiwa kibiashara nchini.
Kampuni hiyo hutengeneza pombe aina ya Summit Lager na Summit Malt miongoni mwa zingine na imetoa ajira kwa wafanyikazi kiwandani, mabaa na wasambazaji.