• Nairobi
  • Last Updated March 19th, 2024 11:34 AM
FUNGUKA: ‘Kifo cha mdudu hunisisimua ajabu…’

FUNGUKA: ‘Kifo cha mdudu hunisisimua ajabu…’

Na PAULINE ONGAJI

BILA shaka tumeumbwa tofauti, kumaanisha kwamba hata katika masuala ya mahaba, vichocheo vyetu ni tofauti kabisa.

Kuna wale wanaochochewa na mguso, huku wengine ashiki ikiletwa na wanachotazama au kuambiwa kabla au wakati wa mahaba.

Lakini kwake Benta, ashiki huchochewa na shughuli ambayo huenda kwa wengi sio kawaida. Bibi huyu hupata msisimko wakati huu akiwatazama wadudu wakipondwapondwa na kufa.

Acha kwanza nikutambulishe kwa binti huyu. Benta ana miaka 33 na ni mfanyabiashara ambapo anamiliki nyumba za kupangisha na magari kadhaa ya uchukuzi viungani mwa jiji la Nairobi.

Ni singo lakini ana watoto wawili. Bila shaka biashara anazomiliki zimemwezesha pamoja na wanawe kuishi maisha ya kifahari.

Kimaumbile, Mungu alikuwa mkarimu kwa binti huyu. Benta ana uso wa kupendeza, sifa inayozidishwa na ngozi yake nyororo na inayong’aa. Aidha, Mungu kamjalia umbo la chupa linalovutia kiasi kwamba ni kawaida kubabaisha madume kila anapotembea.

Mbali na urembo huu, binti huyu ni mweledi chumbani, angaa kulingana na masimulizi ya mchumbake wa sasa, Henry.

Lakini uzuri huu umetiwa doa na kichocheo chake cha ashiki ambacho kwa wengi sio cha kawaida.

“Kwa kawaida mimi hupata msisimko ninapotazama wadudu wakipondwa na kufa. Nazungumzia wadudu ambao wakipondwa watatoa yale majimaji mfano wa usaha, kwa mfano mende na kiwavi yaani caterpillar.

Ashiki yangu haichochewi kwa kutazama wadudu hawa wakipondwa kwa ufagio au kifaa kingine kile; napata msisimko mwenzangu anapofanya hivyo kwa kutumia miguu yake mitupu bila viatu au hata soksi.

Kwa hivyo kabla ya kunivutia lazima uwe tayari kuonyesha kwamba huwaogopi viumbe hawa. Katika deti yetu ya kwanza nitawaleta na lazima uwe unaweza kuwagusa. Huo ndio mtihani wa kwanza.

Katika mtihani wa pili utalazimika kuonyesha ustadi wako wa kuwasaka wadudu hawa na kuwaweka kikapuni. Hii ni muhimu kwa sababu kikapu hicho kikijaa, basi inamaanisha kwamba wakati wa mahaba nitakupandisha mzuka ajabu!

Pindi wanapoisha na unahisi kana kwamba hujatosheka, basi itakubidi kurejea nje na kuwasaka wengine. Ndiposa katika ua langu nimepanda miti inayopendwa na wadudu kama vile viwavi ili ninapowahitaji wanapatikana kwa urahisi.

Aidha, katika jumba langu nimehifadhi chumba kimoja kinachowekwa masalio ya chakula; mazingira mwafaka ya kuwafanya mende wazaane na kuongezeka ili kutumika katika shughuli hii.

Kilichonifanya niwe hivi ni kwamba nikiwa mdogo ndugu zangu walikuwa na mazoea ya kunishtua kwa kutumia hawa wadudu. Hii ilinisababishia hofu ambapo ninapomuona yeyote na hasa mwanamume akiwaangamiza wakati wa mahaba, basi mwili wawaka kama kibatari.

Yeyote anayefanya hivi nami, basi namhakikishia uhondo wa kipekee, ndiposa licha ya masharti haya ambayo kwa wengine ni ya kutisha, wanaume wanaopata fursa ya kuonjeshwa asali ya kibuyu changu kwa kawaida hawataki kuniacha”.

You can share this post!

UMBEA: Si vizuri kuficha hasira, yaweza kugeuka shubiri...

Mwanamuziki nyota wa nyimbo za Country, Kenny Rogers afariki

adminleo