• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 6:55 AM
CORONA: Maafisa mbioni kuhakikisha maagizo yanafuatwa

CORONA: Maafisa mbioni kuhakikisha maagizo yanafuatwa

NA WAANDISHI WETU

MAAFISA wa serikali Jumatatu waliongoza harakati za kuhakikisha raia wanatii maagizo ya kukaa nyumbani na magari kuwabeba abiria wanaostahili.

Maagizo hayo yalitolewa Jumapili na Waziri wa Afya Mutahi Kagwe kama njia ya kuzuia ueneaji wa virusi vya corona ambavyo vimesabisha vifo vya zaidi ya raia 15,300 kote duniani.

Polisi walionekana katika miji mbalimbali wakiam- risha raia waliokuwa wakirandaranda bila sababu warejee nyumbani badala ya kujikusanya kwenye makundi wakipiga gumzo jinsi walivyozoea.

Maafisa wa serikali walizuru miji mbalimbali kuk- agua iwapo magari ya uchukuzi yalikuwa yametii agizo la serikali la kubeba idadi ya abiria iliyostahili.

Japo magari mengi yalitii sheria, abiria nao walilala- mika kutozwa nauli ya juu, baadhi ya wahudumu wak- itoza mara mbili zaidi ya ile nauli ya kawaida.

Mjini Nakuru, Mshirikishi wa Usalama Ukanda wa Bonde la Ufa, George Natembeya aliongoza kampeni ya kukagua matatu na kuamrisha watu waliokuwa wakirandaranda mjini bila kazi maalum warejee nyumbani.

Bw Natembeya aliwataka wakazi kuwa makini na kutekeleza mikakati ya serikali inayopendekeza jinsi ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

“Watu ambao wanatakiwa kuwa hapa ni madereva na utingo wa magari pekee. Utingo wanastahili ku- wapokea abiria na kuwaelekeza kwenye magari yao ili kuchukua muda mchache sana kwenye kituo cha mabasi. Watu wengine wote wasiokuwa na kazi hapa, waondoke mara moja na kuelekea nyumbani,” akaonya Bw Natembeya.

Hali ilikuwa hiyo hiyo jijini Nairobi ambapo magari mengi ya uchukuzi yanayohudumu katika mitaa mbalimbali yalitimiza agizo la serikali.

Matatu za Utimo zinazohudumu kutoka Umo- ja hadi jijini zilifuata masharti ya serikali kwamba abiria watumie asilimia 60 ya viti pekee kama njia ya kuhakikisha kila moja anakaa mbali na mwenziwe.

Hali hiyo ilisababisha kupanda kwa nauli kutoka Sh60 za awali hadi Sh100, utingo wakisema hiyo ndi- yo ilikuwa njia pekee ya kufidia hasara ya viti vingine kusalia bila abiria.

Watu wenye mazoea ya kukongamana barabarani au maeneo mbalimbali jijini Nairobi pia waliagizwa warudi nyumbani na maafisa wa kitengo cha GSU na polisi waliokuwa wakipiga doria mchana kutwa. Polisi mjini Vihiga nao walikuwa macho kuhakikisha magari yalitii agizo la serikali.

Kama tu maeneo mengine, abiria kutoka Vihiga waliokuwa wakielekea Kakamega au Kisumu walilipa nauli ya juu kuliko ka- waida.

Matatu zinazofaa kubeba abiria 14 zilikuwa zikibeba abiria wanane pekee. JIjini Kisumu, Gavana Anyang’ Nyong’o na Kamishi- na wa Kaunti Susan Waweru waliamrisha matatu kutoka Kisii, Migori, Homa Bay, Kericho, Chemelil na Muhoroni kuwashukisha abiria katika kituo cha Mowlem badala ya kufika katikati mwa jiji.

Magari ya uchukuzi yanayohudumu kwenye bara- bara ya Homa Bay-Mbita hata hivyo yalibeba abiria kama kawaida na kupuuza agizo la serikali.

Madereva hata waliongeza idadi ya abiria, baadhi wakionekana kusimama kwa kukosa viti. Wakati uo huo, watu 363 ambao Bw Kagwe alitangaza kwamba walitangamana na wengine wanane walioambukizwa jana walisafirishwa hadi Chuo cha serikali cha Kabete (KSG), jijini Nairobi ili kutengwa.

Watu hao walisafirishwa kwa mabasi ya Shirika la Huduma ya Vijana (NYS).

Ripoti za Phylis Musasia, Cecil Odongo, Derick Luvega, George Odiwuor na Rushdie Oudia

You can share this post!

Hofu Siaya padre akieneza coronavirus

Corona ni shetani, dawa ni kwenda kanisani, msikitini...

adminleo