Mwanamuziki mwingine Afrika afa kwa Covid-19
Na MASHIRIKA
MWANAMUZIKI mashuhuri raia wa Cameroon, Manu Dibango amefariki kutokana na virusi vya corona.
Mwanamuziki huyo wa mitindo ya Jazz, alikuwa amelazwa katika hospitali moja jijini Paris, Ufaransa, baada ya vipimo kuonyesha alikuwa kuwa na coronavirus.
Wiki iliyopita, familia yake iliwahakikishia mashabiki kwamba alikuwa anaendelea kupata nafuu.
Dibango ni mwanamuziki wa pili Afrika kuaga dunia kutokana na corona baada ya Aurlus Mabele kuaga wiki iliyopita.
Baadhi ya vibao maarufu vya Dibango kama vile “Soul Makossa” aliyoirekodi mnamo 1972.
Inadaiwa wimbo huo ulimpa mwanamuziki Michael Jackson shime ya kutunga wimbo wake kwa jina “Wanna Be Starting Somethin’ ” ambao ni wa kwanza kwenye albamu yake ya “Thriller” iliyorekodiwa mnamo 1982.