Habari

KAFYU: Maisha magumu yaanza

March 26th, 2020 Kusoma ni dakika: 2

NA MWANDISHI WETU

RAIS Uhuru Kenyatta Jumatano alitangaza marufuku ya kutotoka nje usiku kote nchini kuanzia Ijumaa ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Rais alitangaza kafyu hiyo wakati idadi ya watu walioambukizwa ilipofika 28, huku mmoja kati yao akithibitishwa kupona kabisa kutokana na virusi hivyo.

Kafyu hiyo itatekelezwa kila siku kuanzia saa moja jioni hadi saa kumi na moja alfajiri, ili kupunguza utangamano baina ya watu na kukusanyika katika makundi.

“Kuanzia Ijumaa ya Machi 27, kutakuwa na kafyu ya kila siku kote katika Jamhuri ya Kenya. Hakuna yeyote atakayeruhusiwa kutembea usiku isipokuwa wanaotoa huduma muhimu,” akasema Rais.

Kafyu hiyo itafanya maisha ya Wakenya kuwa magumu zaidi na kubadili jinsi watu wanavyoishi.

Wafanyibiashara pia wataendelea kuwa na wakati mgumu ikizingatiwa ta- yari wengi wamefunga biashara zao.

Kufuatia kafyu hiyo, magari ya matatu yatasitisha shughuli mapema na bodaboda kufunga ili kuheshimu kafyu hiyo, jambo ambalo litahitaji watu kwenda nyum- bani mapema.

Maduka pia yatafungwa kabla ya saamoja jioni na hivyo watu watu watalazi- mika kujipanga upya. Mara baada ya kutangazwa kwa kafyu hiyo, baadhi ya Wakenya walieleza hofu kuwa maafisa wa usalama na utawala huenda wakachukua fursa hiyo kuhangaisha wananchi.

Mataifa mengine kadhaa yameweka kafyu ya saa 24 katika juhudi za kukabili janga la corona ambalo limesambaa kati- ka kila pembe ya dunia. Afrika Kusini ilitangaza kafyu ya kutotoka nje ya siku 21 kuanzia leo.

Nchi zingine ambazo zimeweka marufuku ya kutoka nyumbani ni Rwanda, Uingereza, Italia, Uhispania miongoni mwa zingine.

Kufikia jana jioni watu elfu 445 waliku- wa wamethibitishwa kuambukizwa kote duniani na elfu 19 miongoni mwao wakia- ga dunia.

Hii ni mara ya kwanza kuwepo kwa kaf- yu ya kitaifa katika historia ya Kenya. Zile ambazo zimekuwepo zimekuwa zikijikita katika maeneo ambayo yamekuwa na ghasia ama matatizo ya kiusalama.

Jiji la Nairobi lilikuwa chini ya kafyu mnamo 1982 baada ya jaribio la jeshi la wanahewa kupindua serikali ya mare- hemu Daniel arap Moi.

Mnamo 2017 serikali ilitangaza kafyu ya usiku katika kaunti za Lamu, Tana River na Garissa kutokana na tisho la magaidi.

Rais Kenyatta alisema serikali haitasita kuchukua hatua kali zaidi, iwapo Wakenya wataendelea kupuuza maagizo ya Wizara ya Afya yanayolenga kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amekuwa akitangaza kanuni ambazo zinapasa kuzingatiwa na kila Mkenya katika juhudi za kukabili usambazaji wa virusi vya corona.

Wakopaji kupumua hadi janga likabiliwe

Wakenya wengi hukopa pesa kutoka kwa mashirika ambayo hutoa mikopo kwa njia ya simu kwa saba- bu hayana masharti magumu kama mikopo ya benki.

Hii hupelekea baadhi yao kukopa kutoka zaidi ya shirika moja na kuji- pata wakishindwa kulipa, hali inay- opelekea majina yao kuorodheshwa katika CRB.

Wanaoorodheshwa hawawezi kukopeshwa na shirika lingine lolote ama benki. Rais Kenyatta pia alitangaza kuondolewa kwa ushuru wa mapato kwa wafanyakazi ambao hupokea mshahara wa Sh24,000 kila mwezi.

“Na kwa wale ambao wanapata mishahara ya juu naamuru Mamlaka ya Ushuru Nchini (KRA) kupun- guza ushuru unaotozwa mishahara yao (PAYE) kutoka asilimia 30 hadi asilimia 25,” Rais akasema.

Vile vile, alipunguza ushuru unaotozwa mapato ya kampuni kutoka asilimia 30 hadi asilimia 25. Rais Kenyatta pia alitoa afueni kwa wafanyabiashara wadogo kwa kupunguza ushuru unaotozwa mauzo yao kutoka asilimia tatu hadi asil- imia moja.

Ushuru huu ulianza kukusanywa na KRA mwezi Januari mwaka huu katika jitihada zake za kuimarisha kiwango cha mapato ya kitaifa.

Vile vile, kiongozi wa taifa alitan- gaza kupunguzwa kwa Ushuru wa Ziada ya Thamani (VAT) kwa bidhaa na huduma zote kutoka asilimia 16 hadi asilimia 14 kuanzia Aprili 1 mwaka huu.

Kufuatia hatua hii, bei ya bidhaa na huduma zinatarajiwa kushuka, japo kwa kiwango kidogo ili kutoa afueni kwa Wakenya wanaokabili- wa na kupungua kwa mapato tangu virusi vya corona vilipothibitishwa nchini.