Makala

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Jinsi unavyotakiwa kutumia alama mbalimbali za uakifishaji

March 28th, 2020 Kusoma ni dakika: 2

Na MARY WANGARI

Herufi kubwa

MAJINA ya vyeo vya watu au heshima kwa mfano: Rais, Naibu Rais, Waziri, Gavana Seneta, Diwani, Profesa, Sheikh, Askofu, Dkt, na kadhalika.

Majina au sifa zinazoandamana na majina ya pekee kama yafuatayo:

Bahari Hindi, Mlima Kenya Bonde la Ufa, Ziwa Victoria, na kadhalika.

Neno lolote litakapopewa hadhi ya pekee.

Kama vile Chama cha Jubilee, Chama cha Maendeleo Chap Chap, Vita vya MajiMaji, Saba Saba na kadhalika

Katika sifa inayotokana na jina la kipekee kama ifuatavyo

Mkenya, Mchina Mhispania, Mwingereza

Katika Akronimu au finyazo za vyama, mashirika jumuia na mengineyo jinsi ifuatavyo:

TUKI, CHAKIMO, BAKITA,

Katika majina ya siku za wiki na miezi

Ijumaa, Jumamosi, Alhamisi, Januari, Septemba, Disemba

Hutumika katika majina ya vitabu na mada kama vile Kifo Kisimani, Mayai Waziri wa Mayai, Walenisi, Uhuru wa Mwandishi, Diwani ya Mnyampala na kadhalika.

Majina ya sayari kama vile: Jua, Zebaki, Zuhura, Dunia, Mirihi, Mshtarii, Zohali, Sarteni, Kausi, Utaridi Chanzo

Majina ya Sikukuu: Pasaka, Krismasi, Jamhuri, Madaraka, Idd Mubarak.

Herufi kubwa hutumika pia katika majina ya nafasi yanapotumika kuleta maana maalum kwa mfano:

Mwamuzi ni Yeye (Mungu)

Alama za uakifishaji zinazotumika katika mwisho wa sentensi

Miongoni mwa alama zote za uakifishaji zinazotumika katika uandishi, yamkini alama zinazotumika katika mwisho wa sentensi ndizo rahisi sana kutumia.

Alama hizi huwekwa mwisho wa sentensi kamili na huweza kuamua iwapo mawazo ya matini katika sentensi itakuwa maelezo au kauli kamili, itaashiria hisia ya mshangao, ghadhabu au furaha au iwapo itakuwa swali.

Alama hizi ni tatu na zinajumuisha

Nukta au Kituo Kikuu (.)

Alama ya Mshangao au ya hisia kali (!)

Alama ya Kuuliza (?)

Nukta au Kituo Kikuu (.)

Hutumika mwishoni mwa neno, tungo au kifungu chenye kuleta maana kamili.

Kwa mfano: Mgonjwa aliyethibitishwa kuwa na virusi vya corona amepata nafuu

Hutumiwa kufupisho maneno au jina refu kwa mfano: K.C.P.E., K.C.S.E., K.A.N.U. Bw. k.v. n.k.

Hutumiwa kutenganisha vitu vinavyohusiana lakini vimo katika vitengo tofauti kwa mfano:

Fedha – 855.50 (shilingi themanini na tano na senti hamsini)

Wakati – 1.45 (saa mbili kasorobo kwa Kiswahili)

Desimali – 0.01 (Sufuri nukta sufuri moja) National Casino: https://onlinekaszinojatekok.com/national-casino/

 

[email protected]

Marejeo

Mkinga, M.G. (2007). Kiswahili Kwa Shule za Msingi 2 (MWL). Dar es Salaam: Educational Books Publishers Ltd.

Norton, S. & Green, B. (2002). Essay Essentials with Reading, Tol. 3. Edinburgh: Thomson Nelson.

Stephano, R. (2015). “Uzingatizi wa Viakifishi katika Uandishi wa Kitaaluma: Mifano kutoka Shule za Msingi Tanzania.” Tasnifu ya Shahada ya Uzamifu ya Chuo Kikuu cha Dodoma (haijachapishwa).