• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
Msiruhusu watoto kutazama video za ngono, wazazi waambiwa

Msiruhusu watoto kutazama video za ngono, wazazi waambiwa

Na MISHI GONGO

AFISA wa watoto katika kaunti ya Mombasa, Bw Philip Nzenge amewaomba wazazi wafuatilie wanachokifanya watoto wao wanapokuwa mitandaoni.

Tahadhari yake inatokana na ongezeko la idadi ya watoto wanaoshiriki video za ngono na kudhulumiwa kupitia mitandao hiyo.

Afisa huyo alieleza kuwa, kufuatia shule kufungwa ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya corona, watoto wanatumia muda wao mwingi katika mitandao, hivyo kuwaweka katika hatari ya kupitia aina mbali mbali za unyanyasaji katika mitandao.

Akizungumza na Taifa jana, Bw Nzenge aliwataka wazazi kuwa waangalifu ili kujua shughuli wanazofanya watoto hao wanapokuwa mitandaoni.

“Kuna mambo mengi machafu yanayoendelea mitandaoni, hivyo ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto wake anatumia mitandao kusoma na si kuangalia mambo yatakayo mpotosha,”akasema.

Bw Nzenge alisema kaunti ya Mombasa imerekodi visa vingi vya ulanguzi wa watoto.

 

  • Tags

You can share this post!

Wakenya wakerwa na kimya cha wanasiasa vigogo

Zaidi ya kesi 3,000 kuamuliwa siku 14 zijazo

adminleo