• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 11:05 AM
Bei ya mafuta taa yapungua kwa Sh18

Bei ya mafuta taa yapungua kwa Sh18

Na Benson Matheka

WAKENYA wamepata afueni baada ya bei ya mafuta kushuka kwa kiwango kikubwa.

Mamlaka ya kuthibiti kawi nchini jana ilipunguza bei ya petroli aina ya Super kwa Sh18, dizeli kwa Sh4.09 na mafuta taa kwa Sh18.18.

Bei za mafuta zimekuwa zikishuka kuanzia Machi mwaka huu. Hatua hii itafanya bidhaa hizi kuuzwa kwa bei ya chini kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Taarifa ya Mamlaka ya kuthibiti kawi ilisema kwanba hatua hii imetokana na kushuka kwa bei za mafuta yasiyosafishwa ulimwenguni mwezi Machi.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Parvel Oimeke, alisema kwamba bei ya petroli mjini Mombasa Kwale itakuwa Sh90.40, dizeli itauzwa kwa Sh95.05 na bei ya mafuta taa mjini humo itakuwa Sh74.82.

Jijini Nairobi, bei ya petroli itakuwa Sh92.87 dizeli itauzwa kwa Sh97.56 na bei ya mafuta taa itakuwa Sh77.28.

Wenye magari kaunti ya Kisumu watanunua petroli kwa Sh93.87, dizeli kwa Sh98.49 na mafuta taa kwa Sh79.

 

You can share this post!

Watu 32 waliotengwa kupimwa corona Mandera watoweka

Kibra na Mombasa maeneo hatari kwa ueneaji wa corona

adminleo