• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Duma na simba waambukizwa virusi vya corona na binadamu

Duma na simba waambukizwa virusi vya corona na binadamu

Na MASHIRIKA na CHARLES WASONGA

DUMA wanne na simba wawili, maarufu kimombo kama, African lions, wamepatika na virusi vya corona katika hifadhi ya wanyama kwa jina, Bronx Zoo iliyoko jijini New York, Shirika la kutetea Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) imefichua.

Shirika hilo lisilo la faida, ambalo linaendesha hifadhi hiyo, lilisema duma watatu na simba hao walianza kuonyesha dalili ugonjwa huo mapema Aprili.

Kulingana na wasimamizi wa WCS walisema wanyama hao wamekuwa wakikohoa ishara kwamba wameambukizwa na ugonjwa huo ambao umewaua maelfu ya watu kote ulimwenguni.

Walieleza kuwa wanyama hao waliambukizwa virusi hivyo na mfanyakazi mmoja wa hifadhi hiyo ambayo wakati huo hakuwa ameanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo maarufu kama Covid-19.

Kufuatia kisa hicho wakuu wa hifadhi ya Bronx Zoo sasa wameweka kanuni kali ambazo wanapasa kuzingatia wanapowatunza wanyamapori hao. Kanuni hizo za kuzuia maambukizi pia zitazingatiwa katika hifadhi zingine zinazosimamiwa na shirika la WCS katika jimbo hilo.

Miongoni mwa duma ambao ambao waliambukizwa ugonjwa huo ni yule anayetambuliwa kwa jina Nadia ambaye ni wa asili ya Malaysia na ambaye ana umri wa miaka minne.

“Hatujui namna ugonjwa huu utaathiri wanyama hawa ikizingatiwa kuwa wanyama huathirika kwa njia tofauti na virusi vya corona. Lakini tutawachunguza kwa makini huku tukiwatibu hadi wapone,” akasema Daktari mkuu wa wanyama katika hifadhi hiyo Paul Calle, kwenye ujumbe katika ukurasa wake wa Facebook.

Kulingana na kanuni zilizotolewa na Bronx Zoo, mtu yeyote ambaye amebainika kuwa na virusi vya corona anashauri kutotangamana na wanyama hao.

You can share this post!

Kinyozi asimulia anavyokabiliana na hali ngumu ya uchumi

Tutawanyaka wote waliotoroka karantini – Uhuru

adminleo