• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 6:50 AM
KUKABILIANA NA CORONA: Wanafunzi wa JKUAT waunda mitambo miwili ya sola

KUKABILIANA NA CORONA: Wanafunzi wa JKUAT waunda mitambo miwili ya sola

Na LAWRENCE ONGARO

CHUO cha Jomo Kenyatta ( JKUAT), eneo la Juja, Kaunti ya Kiambu, kimeonyesha ubunifu wa kuunda mitambo miwili tofauti aina ya sola.

Mmojawapo wa mitambo hiyo ni aina ya sola inayotumika kidijitali ambayo ikiunganishwa kwa mitambo ya kuleta hewa, pia inakadiria aina ya viini vya Covid-19.

Mtambo mwingine ni wa kunawa mikono kupitia umeme.

Naibu Chansela wa JKUAT Prof Victoria Ngumi anasema ubunifu huo wa kipekee ni kazi ya wanafunzi wa chuo hicho wanaobobea katika taaluma za teknolojia na uhandisi na wanaozama kufanya utafiti wa hali ya juu.

Mmoja wa wanafunzi hao katika ubunifu huo, Bw Karanja Kabini, anasema mitambo hiyo ni za kipekee na kulingana na jinsi ilivyoundwa, inaendeshwa kwa wiki mbili mfululizo bila kufanyiwa marekebisho yoyote ya kimitambo.

“Mtambo wa kuongeza hewa unaendeshwa kidijitali ambapo vidhibiti viko vya ama kupunguza hewa au kuongeza kulingana na hali ya mgonjwa. Pia unaweza ukatumika kwa wakubwa na vilevile kwa wadogo,” akasema Bw Kabini.

Prof Ngumu, anasema wanafunzi hao wa kitengo cha uhandisi wana uwezo wa kuunda mitambo ya kusaidia wagonjwa kupumua – ventilators – kwa wiki moja.

Uzinduzi huo ulifanyika Jumatano katika bewa kuu eneo la Juja na kuhudhuriwa na wahadhiri na wageni kadha kutoka jijini Nairobi na vyuo vingine.

“Uvumbuzi wa aina hiyo utaendelezwa na wanafunzi hao hata wakati serikali itaweza kukabiliana na homa ya corona. Wataendelea kufanya utafiti ili kujiendeleza zaidi katika masomo yao,” akasema Prof Ngumi.

Mtambo huo wa kipekee umebuniwa na wanafunzi, Victor Muthembwa, Boniface Bundi, na Crispus Nyaberi ambao wameamua kuonyesha ujuzi wao kwa lengo la kujitambulisha kama wahandisi wabunifu.

Mwanafunzi Bw Willy Toumbi wa kutoka nchini Cameroun ndiye aliyeongoza kikosi hicho cha wanafunzi kuunda mitambo hiyo miwili.

“Lengo letu kuu ni kuunda mitambo ya kidijitali ambayo inastahili kurahisisha kazi kwa wauguzi wanapotumia mitambo hiyo,” akasema Bw Bundi ambaye ni mmoja wa wanafunzi hao.

Wanafunzi hao wanasema mtambo wa kutumiwa kunawa mikono pia ni wa kipekee ambao unaweza kutumika hata maeneo kavu ya bara Afrika.

Mwenyekiti wa kitengo cha klabu cha ubunifu Bw Reine Katte, kutoka nchini Benin anasema ajenda yao kuu kwa sasa ni kuona ya kwamba ifikapo mwaka wa 2063 kazi 1 milioni zitakuwa zimebuniwa barani Afrika kupitia ubunifu.

Watafiti kutoka vitengo vya afya, na teknolojia ya habari na mawasiliano, wamefungua tovuti itakayowasaidia kufuatilia jinsi homa ya corona inavyoenea sehemu tofauti hapa nchini.

You can share this post!

COVID-19: Kombe la Enterprise kutupwa kando kupisha raga ya...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Alama ya kistari kifupi, ritifaa...

adminleo