• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
DAU LA MAISHA: Aliacha kazi ya kuajiriwa akaanzisha kampuni ya huduma za usafiri

DAU LA MAISHA: Aliacha kazi ya kuajiriwa akaanzisha kampuni ya huduma za usafiri

Na PAULINE ONGAJI

ALIAMUA kuacha kazi ya kuajiriwa na kuanzisha kampuni yake ya usafiri.

Jina lake ni Vidya Jethwa, 39, Meneja Mkurugenzi wa Globetrotter Agency Limited, kampuni ya usafiri ambayo iko katika harakati za kuweka alama katika sekta hii humu nchini na mbali.

Huu ukiwa mwaka wake wa sita tangu kujitosa katika ujasiriamali, kwa sasa kampuni hii imeajiri wafanyakazi 20, huku ikiendesha shughuli zake katika eneo la Parklands, jijini Nairobi.

Ukakamavu na ushupavu wake katika nyanja hii umemfanya kuteuliwa mara tatu katika tuzo za Asian weekly achievers awards.

“Japo sijashinda tuzo hii, nimebahatika kuteuliwa mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka wa 2017 na niliteuliwa tena mwaka wa 2018, vilevile mwaka huu wa 2020,” aongeza.

Basi nini kilichomchochea?

“Tangu utotoni nilikuwa nafurahishwa kila nilipowatazama wahudumu wa ndege wakiwashughulikia wateja, na hapo ndipo ndoto yangu ya kujitosa katika taaluma hii ilipojitokeza,” aeleza.

Hii ilimsukuma kusomea uhudumu wa ndege akiwa chuoni na hata kutafuta ajira katika nyanja hii, suala lililompa ufahamu zaidi.

“Nilipokuwa nikifanya kazi kama mhudumu wa ndege nilielewa mahitaji ya wateja na uwezo wa kusaidia katika hali yoyote ile iliyowakumba,” aeleza.

Lakini haikuwa rahisi kubadili taaluma huku akikumbwa na changamoto mbalimbali.

“Changamoto ya kwanza ilikuwa wakati wa kujiunga na sekta hii ya usafiri. Nakumbuka wakati huo sio wengi waliotaka kumuajiri mtu ambaye hakuwa na tajriba. Nusura nipoteze matumaini, lakini kabla ya kufa moyo nilibahatika kupata kazi kama mhudumu wa ndege,” aeleza.

Kwa sasa anakumbana na changamoto mbalimbali za kikazi.

“Changamoto kuu imekuwa kuwaridhisha wateja; na mammbohuwa mabaya hata zaidi hasa ikiwa ni mteja msumbufu,” asema.

Pia, anasema changamoto nyingine ni kuwa shirika hili bado ni changa; kumaanisha kwamba sio watu wengi ambao wamesikia kuwahusu.

“Aidha, Wakenya wana chaguo nyingi na hivyo masharti ya kupokea huduma ya hali ya juu ni mengi. Hii inamaanisha kwamba lazima tujitahidi kukabiliana na ushindani mkali,” asema.

Lakini hivi kamwe havijazima ndoto na azma yake ya kuthibitisha usemi wa kampuni hii katika sekta ya usafiri.

Kulingana naye ana matumaini makuu kuhusiana na siku zijazo, hasa mara janga la maradhi ya Covid-19 litakapodhibitiwa.

You can share this post!

MWANAMKE MWELEDI: Anathamini na kutambua umuhimu wa sayansi...

KPL kuamua hatima ya ligi wiki hii

adminleo