Wakazi lamu wakiuka kanuni za Covid-19 wakisherehekea Idd
NA KALUME KAZUNGU
Wakazi wa Lamu walikiuka mikakati iliyowekwa kupambana na ugonjwa wa Covid-19 huku wakisherehekea sikukuu ya Idd-ul-Fitr.
Ramadhani ya mwaka huu imewalazimu waislamu kutohudhuria maombi misikitini au kutangamana ili kuzuia kuenea kwa virusi vya corona, lakini wakati wa sherehe, walijumuika pamoja na kuvunja kanuni ya kuweka umbali wa mita moja unusu.
Taifa Leo imegundua kuwa kwa wiki nzima, wakazi wengi wamekuwa wakijazana madukani wakinunua vyakula na nguo ili kufurahia Eid-ul-Fitr, licha ya kuonywa dhidi ya kufanya hivyo na wenye maduka.
Hata hivyo, kufikia sasa, Lamu haina kisa chochote cha Covid-19, sawa na kaunti jirani za Tana River na Garissa.