• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Real Madrid yaendelea kuongoza kwa utajiri duniani – utafiti 

Real Madrid yaendelea kuongoza kwa utajiri duniani – utafiti 

Na MASHIRIKA

KULINGANA na ripoti ya mwaka 2020 ya utafiti uliofanywa na shirika la KPMG, klabu ya Real Madrid inaongoza kwa thamani ya Sh412 bilioni, kiasi ambacho kinawaweka mbele ya Manchester United na Barcelona, huku ikiripotiwa kwamba faida yake iliimarika kwa asilimia nane.

Ripoti hizo zimesema kuimarika kwa vigogo hao wa La Liga kumetambuliwa kati ya 2016-2020, wakati walitwaa Kombe la Mabingwa mara tatu, mbali na faida nyingine ya asilimia 41 iliyopatikana kutokana na biashara yake.

Kulingana na utafiti huo timu 10 bora ni: Real Madrid, Manchester United, Barcelona, Bayern Munich, Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur, Paris Saint-Germain halafu Arsenal.

You can share this post!

David Rudisha nje wiki 16 baada ya upasuaji

Wanataekwondo wa kwanza kabisa wa Kenya katika Olimpiki...

adminleo